Jesca azidi kuonyesha makali | Mwanaspoti

NYOTA wa JKT Stars, Jesca Ngisaise ameendelea kutikisa kwenye Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam BD) akifunga pointi 38 kwenye mchezo dhidi ya Pazi Queens kwenye Uwanja wa Donbosco Oysterbay.

Jesca alifunga pointi hizo katika maeneo ya mitupo mitatu ‘three points’ 18 na ‘asisti’ saba, akifuatiwa na Wade Jaha aliyefunga pointi 12, huku udakajiĀ  ‘rebound’ alidaka mara tano.

Kwa upande wa Pazi Queens, Maria Bonventura alifunga pointi 19, akifuatiwa na Maria Mbena aliyefunga 15.

Katika mchezo huo, JKT Stars iliongoza robo zote nne kwa pointi 16-12, 16-13, 18-11 na 13-11.

Katika michezo mingine, Chui iliifunga Ukonga KingsĀ  kwa pointi 65-64, UDSM Outsiders ikaifunga ABC pointi 67-52 na Tausi Royals ikaifunga Polisi Stars kwa pointi 53-44.

Related Posts