Mkuu wa Dawati awaasa wanafunzi kuhudhuria Masomo kikamilifu,awasihi walimu kufuatili mienendo ya watoto

Katika kuhakikisha watoto wanapata elimu na kusikilizwa kero zao zinazowakabili wanafunzi katika Wilaya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Mkuu wa dawati la jinsia na watoto wilaya hiyo ameendelea kutoa Elimu ambapo amefika katika Shule ya Msingi Kanindo ambapo amewataka wanafunzi kuhudhuria kikamilifu masomo yao huku akiwataka walimu kufuatilia changamoto za wanafunzi hao ili kuzifahamu na kuzitatua.

Mkuu wa dawati hilo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Irene Mayunga ameongeza kuwa walimu wanayonafasi kubwa kuzitambua changamoto wanazopitia wanafunzi kutokana na muda mwingi kukaa na watoto hao ambapo amewaomba kushirikiana kwa karibu na dawati hilo ili kuzimaliza changamoto za ukatili pindi zinapotokea.

A/INSP Irene amewaomba wanafunzi hao kutokukaa kimya pindi wanapoona ama kufanyiwa vitendo vya ukali huku akiwaomba kuzifikisha kwa walimu wao ama viongozi wa dini ili wachukuliwe hatua za kisheia watakao bainika kufanyia ukatili wanafunzi hao.

Nae koplo wa Jeshi la Polisi Agnes amewaomba wanafunzi hao kutambua endapo watasema juu ya vitendo vya ukatili itawasaidia kujiamini na kufaulu katika masomo yao akiwaomba kuendelea kuzitumia klabu za kupinga ukatili mashuleni kuwasilisha kero zao ili zichukulie hatua.

Koplo Stella akatumia fursa hiyo kuwakaribisha walimu katika dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Nyamagana kupata elimu katika masuala mabalimbali juu ya ukatili na vitendo vya ukatili ili kuwa na uelewa wa vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika Jamii.

Related Posts