Netanyahu awasili mjini New York atarajiwa kutoa hotuba hii leo mkutano mkuu wa UN

Wakati waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, awasili mjini New York siku ya Alhamisi kabla ya hotuba yake kwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, uliopangwa kufanyika Ijumaa asubuhi, huku waandamanaji wanaopinga vita huko Gaza wakikusanyika karibu na makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Kundi moja la watu waliopeperusha bendera za Israel na mabango ya kampeni walijieleza kuwa muungano usio rasmi wa mashirika ya Kiyahudi na Israel yanayochukua msimamo wa kupinga uvamizi na vita kuhusiana na maeneo ya Palestina. Walikusanyika karibu na jengo la Umoja wa Mataifa huko Manhattan kupinga kuwasili kwa Netanyahu baada ya kuruka kutoka Israel usiku kucha.

Ilipoanza kunyesha, mzungumzaji alihutubia umati wa watu wapatao 50, akitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano huko Gaza na kuwaambia waliokusanyika kwamba “Netanyahu ataudanganya ulimwengu” siku ya Ijumaa, “kama vile anavyotudanganya sisi Waisraeli”.

“Acheni kuua watoto, malizeni vita, saini makubaliano, warudisheni mateka nyumbani,” msemaji aliendelea kusema. “Hakuna suluhisho la kijeshi.”

Maandamano zaidi yamepangwa kufanyika Alhamisi jioni, Ijumaa na Jumamosi.

Watu walibeba mabango yaliyosomeka “walete mateka nyumbani” na “maliza vita”, na jina la Netanyahu lilipotajwa kwenye hotuba, umati uliimba “aibu, aibu, aibu”.

Related Posts