Mwanafunzi ahukumiwa viboko 12, fidia laki tano kwa kubaka na kulawiti

 

MWANAFUNZI Hija Hamis Msumi (16), anayesoma kidato cha tatu na mkazi wa Nyanjati, Rufiji, amehukumiwa kuchapwa viboko 12 na kulipa Sh. 500,000 kama fidia, baada ya kutiwa hatiani kwa kumbaka na kumlawiti mtoto wa darasa la nne, mwenye umri wa miaka 12 (jina limehifadhiwa). Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Alitenda kosa hilo kati ya Agosti na Novemba, 2023 katika Kijiji cha Nyanjati wilaya ya Kibiti, katika Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya Kibiti, Florian Peter Ntulo, jana tarehe 26 Septemba 2024.

Upande wa mashitaka uliwasilisha mahakamani hapo mashahidi saba (7) pamoja na ushahidi wa nyaraka mbili (2), katika shitaka hilo lililokuwa na makosa mawili ya kubaka na kulawiti.

Baada ya kutiwa hatiani, mshitakiwa alihukumiwa kuchapwa viboko 12 makalioni mbele ya Mahakama kwa makosa yote mawili.

Aidha, Mahakama imemuamuru mshitakiwa kumlipa mwathirika fidia ya Sh. 500,000, kwa madhara aliyomsababishia.

Adhabu ya kuchapwa viboko 12 imetekelezwa mbele ya Mahakama jana tarehe 26 Septemba 2024.
Wakati huo huo, mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Omary Said Lindu (46), mkazi wa Jaribu Mpakani, wilayani humo, kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba, mwenye umri wa miaka (13).

About The Author

Related Posts