Biteko Aipongeza Alaf Kwa Huduma Bora

Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Alaf Limited Tanzania, Hawa Bayumi (kulia) wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa  ya Viwanda (TIMEXPO 2024) yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Michuzi tv

NAIBU Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko ameelezea kuridhishwa na huduma na bidhaa za Alaf Limited Tanzania na kuitaka kampuni hiyo iendelee kuzingatia ubora.

Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonyesho ya Kimataifa ya Viwanda (TIMEEXPO 2024) aliyoyafungua rasmi katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Septemba 26,2027 ǰijini Dar es Salaam na yatamalizika Oktoba 2, 2024.

“Nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya na pia Kwa kushiriki katika Maonyesho haya makubwa,” amesema.

Aidha Dkt. Biteko alihitaji kufahamu ikiwa suala la umeme kiwandani hapo lilishashugulikiwa baada ya kuwepo na malalamiko ya kukatikakatika kwa umeme mara Kwa mara, jambo ambalo lilikuwa linaathiri uzalishaji.

“Mheshimiwa tunakushukuru mno maana suala hili limeshashugulikiwa na sasa uzalishaji unaendelea vizuri,”alijibu Hawa Bayumi ambaye ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Alaf.

Meneja huyo pia ameipongeza serikali kwa kuhakikisha kuwa mazingira ya uzalishaji na biashara kwa ujumla ni mazuri.

“Tunatoa wito kwa serikali iendelee kuboresha mazingira haya zaidi ikiwemo kuangalia sera ambazo sio rafiki kwa wazalishaji na pia kuweka miundombinu sawa ikiwemo barabara ili usafirishaji uwe rahisi,” alimueleza Naibu Waziri Mkuu.

Ameeleza kuwa Alaf itaendelea kutoa suluhisho sahihi ya ujenzi kwa ujumla ikiwemo kuja na teknolojia mpya kama inayotumika kujenga maghala ya nafaka Mkoani Ruvuma ambayo imezingatia ubora wa hali ya juu na ni mpya kabisa.

Related Posts