WANAHARAKATI- MFUMO DUME CHANZO CHA KAZI ZISIZO NA UJIRA

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

WADAU wa Semina za Jinsia na Maendeleo wamepaza sauti zao kukemea Mfumo dume ambao umekuwa nisababu kubwa inayochangia Vijana na wanawake kufanya  kazi zisizo na stara wala ujira ambapo imechangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili na kusababisha magonjwa ya kuambukiza.

Akizungumza Septemba 25,2024 kwenye semina hizo zinazofanyika kila Jumatano  katika ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP, Mwezeshaji mada Bw. Nelson Munisi amesema Mwanamke amekuwa muhanga wa kufanya kazi zisizo na ujira pamoja na stara kutokana na mtazamo hasi wa jamii.

Amesema kazi zisizo na ujira pamoja na stara zimekuwa zikichangia, ongezeko la idadi kubwa ya watu maskini na kupelekea changamoto ya afya ya akili kutokana na kutopewa malipo yeyote kwenye kazi hizo.

Aidha ameeleza kuwa vijana na wanawake wakiwezeshwa kiuchumi itakuwa suluhisho kubwa ambalo litasaidia wasijiingize kufanya kazi zisizo na stara kama kujiuza mwili ili kujipatia kipato.

Pamoja na hayo,ameshauri kuwa Jamii inapaswa kuthamini majukumu yanayofanywa na mwanamke  nyumbani ikiwa ni pamoja na suala la malezi ambapo itasaidia kulinda utu wake katika familia.



Related Posts