BARABARA YA CD MSUYA MWANGA KUWEKWA LAMI KM 4.8..

Na WILLIUM PAUL, MWANGA

SERIKALI imetoa fedha Bilioni 12.8 kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami Barbara ya mchupuko ya CD Msuya kilomita 4.8 Kati ya kilomita 13.8 wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na wananchi wa Mwanga ambapo wamesema kuwa, kukamilika kwa barabara hiyo ya Mchepuko ya CP Msuya yenye kilomita 13.8 kwa kiwango cha lami kitakuza uchumi na kuondoa umasikini kwa kuboresha sekta ya usafirishaji na uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Wakizungumza jana mara baada ya kutembelewa na kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi mkoa, akiwemo Hawa Hamis, alisema barabara hiyo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja moja.

“Tunatoa rai yetu kwa serikali kuhakikisha inakamilisha barabara hiyo kwa wakati na wakati wa utekelezaji, wakandarasi waone namna ya kuwatumia vijana wetu ili waweze kupata ajira, “alisema Husen Mvungi

Akisoma taarifa ya hali ya mradi meneja wa wakala wa barabara Vijijini na mijini TARURA, Mhandisi Musa Sumbwe alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi minne unaotekelezwa kwa fedha ya tozo za Mafuta kwa mwaka 2023/24 na unatekelezwa kwa awamu.

” Awamu ya kwanza ulianza January 04 2023, na kukamilika Julai 8 2024 kwa gharama ya Bilion 4.9 na kazi zilizofanyika ni kusafisha eneo la barabara km 4.8, kuweka tabaka la changarawe Km 2.0 na ujenzi wa madaraja ya wastani ( Box Calvert ) 16, Mradi huu umekamilika na upo kwenye eneo la matazamio,”alisema Mhandisi Sumbwe.

Mhandisi Sumbwe alisema katika mwaka wa fedha 2024/25 serikali imetoa tena fedha Bilioni 12.8 kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kilomita 4.8 ambapo tayari wameshasaini mkataba na Mkandarasi na anatakiwa kuanza kazi sasa.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kwa kutaongeza eneo la makazi na kupunguza msongamano wa magari na kuchochea shughuli za kiuchumi na kukuza mandhari ya mji wa ya mji huo.

Aidha akipokea taarifa hiyo, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (MNEC) kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Seleman Mfinanga wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ambapo aliwataka wakandarasi kushirikiana na wananchi na wafanyabiashara wilayani huo ili kuleta matokeo chanya katika kunufaika na fedha zinazoendelea kuletwa.

“Tunatambua fedha zitaendelea kuja katika kukamilisha barabara hii, shirikianeni na wafanyabiashara waliopo humu na kutoa ajira kwa vijana waliopo humu ili kukuza vipato vya mtu mmoja mmoja na jamiii,”alisema Mfinanga



Related Posts