Ziara ya SADC Live Your Dream maandalizi yafikia pazuri

Wakati siku zikiyoyoma za kuelekea kwenye Ziara ya Barabarani inayodhamiria kuonesha ndoto za wengi zenye mitazamo chanya yenye kuleta utofauti kwenye jamii mengi yatarajiwa huku maandalizi yakitajwa kukamilika hivi karibuni

Ziara ya Barabara ya SADC Live Your Dream ni tukio muhimu ambalo litalenga kukuza ubadilishanaji wa utamaduni, kujieleza kwa nia ya sanaa, Utalii wa SADC na uwezeshaji wa kiuchumi katika kanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na inatarajiwa kuanza Octoba 17 hadi Novemba 18 mwaka huu.

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Afrika Speaks/GAAB Munyaradzi Muzenda amesema kwa kusafiri katika nchi mbalimbali, ziara hii itakuza ujumuishaji wa mawazo, maono, ndoto, talanta na umoja,lakini utofauti, na kutoa jukwaa kwa wasanii, wajasiriamali, na wavumbuzi kuonyesha vipaji na bidhaa zao.

 

Ziara hiyo pia inalenga kuenzi na kusherehekea hadithi za nguli wa SADC Wanaoishi kwa kuanzia na nchi zinazopitia misafara kwa kuwahamasisha vijana kufuata na Kuishi ndoto zao.

Ni safari ndefu ya kuzingatia suluhu ya SDGs lakini pia ziara hiyo itashirikisha msafara wa magari yenye chapa zilizobeba dhima muhimu ikiwa ni pamoja na Land Rover yenye chapa ya Zimbabwe, inayosafiri katika nchi za SADC.

 

 

 

 

 

Related Posts