Uzoefu waiponza Cosmopolitan | Mwanaspoti

KICHAPO cha mabao 2-0, ilichokipata Cosmopolitan wiki iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar, kimemfanya kocha mkuu wa kikosi hicho, Mohamed Kijuso kudai sababu zilizowanyima ushindi ni wachezaji kukosa uzoefu tofauti na washindani wao.

Timu hiyo imekumbana na kichapo hicho cha kwanza msimu huu, baada ya mchezo wa ufunguzi kutoka sare ya bao 1-1, dhidi ya African Sports.

“Tulicheza na timu nzuri na yenye wachezaji wazoefu zaidi yetu, tuliruhusu mabao ya haraka ila nashukuru tulistahimili na kurudi mchezoni, ni mchezo wa pili hivyo tunaendelea kuufanyia kazi upungufu uliopo hasa eneo letu la kujilinda.”

Kocha huyo aliongeza, bado hakuna balansi nzuri ya kuzuia na kushambulia hivyo anarudi katika uwanja wa mazoezi kufanyia kazi changamoto hiyo, huku akiwaomba mashabiki kuipatia sapoti kikosi hicho akiamini msimu huu utakuwa bora zaidi kwao.

Kijuso anayekiongoza kikosi hicho kwa msimu wa pili sasa katika Ligi ya Championship, msimu uliopita aliiongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya tisa na pointi 39, baada ya kushinda michezo 11, sare sita na kupoteza 13 kati ya 30 iliyocheza.

Related Posts