UDUMAVU KWA WATOTO WAPUNGUA KWA ASILIMIA 30

 

 

MWANDISHI WETU

MIKAKATI na nguvu zinahitajika ili kupunguza udumavu nchini licha ya tafiti ya mwaka 2022 kuonesha kupungua kwa asilimia 30 kutoka asilimia 50 kwa mwaka 1972.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mtaalamu wa Lishe na Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Lishe Tanzania, Ester Nkuba katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa vyombo mbalimbali nchini  ili waweze kuandika taarifa zinazohusu lishe kwa usahihi.

“Ukiangalia mizania unaona imepungua ingawa ikilinganisha na takwimu za kimataifa bado nguvu inahitajika kuendelea kuipunguza pia ukiangalia utapiamlo kwa upande wa uzito uliokithiri (viriba 

tumbo) kwa mwaka 1972 takwimu zinaonesha ilikuwa ni asilimia 11 na sasa imefika 36 asilimia kwa maana inazidi kupanda”.

“Wito wangu ni kwamba licha ya Serikali kuendelea na jitihada za kupambana ili kuhakikisha utapiamlo unakoma Tanzania, wadau na sekta mbalimbali nchini wanatakiwa kuunganisha nguvu ya pamoja jambolitakalosaidia elimu ya kutosha kutolewa kwa jamii itakayoyafanya kutekeleza namna ya inavyohitajika kula vyakula mchanganyiko kutoka katika makundi sita,”amesema.

Ameongeza kuwa ikiwa elimu itafika kwa usahihi kwa wananchi na kutumika vizuri itasaidia watoto wanaozaliwa kupewa maziwa na mama pekee kwa maana yanavirutubishi vyote vinavyohitaka bila kupewa chakula kingine na anafika miezi anaanza kupewa chakula mchanganyiko kutoka kwenye makundi hayo.

Nkuba akifafanua kuhusu makundi hayo amesema kundi la kwanza ni la nafaka, mazoa ya mizizi na ndizi mbivu linalosaidia kuupa mwili wanga na nguvu.

Kundi la pili ni la vyakula vyenye asili ya nyama ikiwemo samaki, nyama, maziwa hapo inapatikana protini ambayo inasaidia ukuaji wa mtoto.

Pia anasema kundi la tatu ni vyakula vyenye asili ya jamii ya kunde na mboga, hapo inapatikana protini inayotokana na mimea ambayo ni muhimu zaidi katika mahitaji ya mwili na kundi la nne ni matunda ambalo linasaidia kupatokana kwa madini na vitamini ambayo ni muhimu kwa ajili ya kupambana na utapiamlo ya aina ya tatu ambayo ni upungufu wa virutubishi.

Aidha ametaja kundi la tano ni linalohusu vyakula vyenye asili ya mbogamboga, hapo inapatikana vitamini kwa wingi na madini yanayosaidia kujikinga na magonjwa mbalimbali na kundi la mwisho  ni la 

Related Posts