MIAKA 25 YA HUDUMA YA MTOTO WAZAZI WAPEWA NENO.

Wazazi na walezi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao nyakati zote katika kuhakikisha wanakuwa na maadili mazuri ili kupunguza matukio ya unyanyasaji na ukatili kwa watoto

Wito huo umetolewa na Diwani viti maalumu Tarafa ya Mbugwe Wilaya ya Babati Mkoani Manyara Bi Naomi Sangu Wakati wa Maadhimisho ya miaka 25 ya Huduma ya mtoto na Kijana, Ambapo amesema wazazi na walezi wanatakiwa kuwalea watoto katika misingi mizuri, ikiwa ni pamoja na kujenga urafiki na ukaribu ili waweze kutambua changamoto wanazozipitia na kuzitatua

Amesema miongoni mwa sababu kubwa za ukatili kwa watoto ni wazazi na walezi kukosa ukaribu na watoto wao jambo ambalo linawafanya wasitambue changamoto zinazowakabili na kuzitatua kwa haraka”Yawezakana mambo mengi mabaya yanatokea yanaendelea kutokea, yanaendelea kufanyika kwa sababu wazazi Tumekosa Masikio ya kusikiliza kile ambacho watoto wanaotuambia”

 

” Siku zote  ukitaka kujua siri, ukitaka kupata jambo kwa mtoto fanya Urafiki na mtoto, ukifanya urafiki na mtoto utapata mambo ambayo hata hukuwahi kuyatarajia

Ameongeza kuwa kumwadhibu mtoto pekee Haitoshi bali kuwa naye karibu ni njia nyingine nzuri zaidi ya kufanya mtoto kuwa salama

Kwa upande wake Sara Mwanjoka ambaye ni mwezeshaji Compassioni Klasta  ya Magugu na Monduli amelishukuru Kanisa klasta ya Magugu kwa ushirikiano mzuri waliouonyesha na shirika la Compassion Internatinal Tanzania kwa  takribani miaka 25 katika kuwalea watoto na vijana katika maadili Yaliyo Bora

Akisoma hotuba kwa niaba ya mkurugenzi wa shirika la Compassion Tanzania Marry Lema,Bi Sara amesema katika vituo vitano kutoka katika klasta ya Magugu shirika la Compassion linatekeleza huduma hiyo kuhakikisha vijana na watoto wanapata elimu na kuzifikia ndoto zao ambapo zaidi ya Million 522  hutumwa  katika vituo hivyo kuwapatia vijana taaluma na ujuzi wa kujiajiri ambapo baadhi ha vijana wameweza kujiajiri katika fani mbalimbali

 

Nao Baadhi vijana waliofanikiwa kujiajiri kupitia Fani Mbalimbali wamelishukuru shirika la Compassion kwa kuwawezesha kujipatia taaluma na ujuzi wa kujiajiri

Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni “Malezi Bora kwa Ulinzi wa mtoto” ambapo Imelenga kuimiza jàmii kutekeleza wajibu wa kimalezi ili kuimarisha ulinzi na ustawi wa mtoto wa kitanzania bila kujali jinsia, sura, Rangi,Dini  ama kabila lake

Related Posts