Said Jr amfuata Msuva Iraq

KIUNGO Mshambuliaji kinda wa Tanzania, Said Khamis ‘Said Jr’ amepata shavu la kusajiliwa Peshmarga Sulaymaniya SC inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Iraq akiungana na Simon Msuva anayetumikia Al Talaba.

Nyota huyo amesajiliwa na timu hiyo akitokea FK Jedinstvo ya Serbia iliyokuwa inashiriki Ligi daraja la kwanza nchini humo.

Mwanaspoti linafahamu kuwa mshambuliaji huyo amepewa mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia mabingwa hao wa zamani wa ligi ya Iraq msimu 2009/10.

Baada ya tetesi hizo Nje ya Bongo ilimtafuta kufahamu kuhusu dili akisema kwa sasa sio muda wa kuzungumza akisisitiza muda sahihi ukifika ataongelea.

“Mambo yakiwa mazuri nitazungumza lakini kwa sasa tuache kwanza mambo yakikamilika watu watajua kwa kuwa tayari timu nimepata,” alisema Said Jr

Timu ya Peshmarga ilicheza katika Ligi daraja la kwanza msimu wa 2009/10 na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi hiyo iliyowapandisha hadi ligi kuu.

Baada ya kupanda ikafanikiwa kucheza Ligi Kuu nchini Iraq msimu wa 2010/11 ikicheza katika Kundi la Kaskazini.

Hata hivyo timu haikuwa na uwezo wa kutosha, na licha ya kubadilisha kocha, timu iliendelea kupoteza mechi zake na msimu ulipotamatika ilishushwa daraja kurudi katika Ligi ya daraja la Kwanza.

Related Posts