Hukumu ya kesi ya Nyundo na wenzake wanne kutolewa leo

Hukumu ya kesi ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam inayowakabili washtakiwa wanne wakiwamo askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wa Magereza, itatolewa leo Jumatatu, Septemba 30, 2024.

 

Kesi hii ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 inawakabili washtakiwa wanne akiwamo MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo ambaye ni askari wa JWTZ, askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Katika kesi hii maarufu ‘waliotumwa na afande’ imesikilizwa faragha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi 18 na vielelezo 12 kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa.

 

Washtakiwa walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 19, 2024 na kusomewa mashtaka mawili ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti huyo ambaye mahakamani anatambulika kwa jila la

XY.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Zabibu Mpangule washtakiwa hao baada ya kusomewa mashataka walikana na kutokana na unyeti wa kesi hiyo hawakupatiwa dhamana.

Related Posts