DC Linda Salekwa abariki mashindano ya Pool Table….

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa ambaye pia ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Mchezo wa Pool Table yaliyoandaliwa na Kampuni ya Ryan Company nakufanyika siku ya Leo Mtaa wa Summer Night ili kutafuta Washindi wanne wa Mchezo Huo Mjini Mafinga.

Dkt Linda Salekwa Ameupongeza Uongozi wa Ryan company kwa Kuandaa mashindano hayo Sambamba na kuwataka Wananchi kucheza Mchezo huo Mara baada ya Mda Wa Kazi.

Sambamba na hayo Mhe Linda Salekwa amewasihi Vijana na wajitokeze Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 pamoja na kugombea nafasi mbalimbali katika Jamii zao.

Mchezo wa pool ni kati ya michezo inayopendwa sana na vijana. Pool huwa na bodi yenye vijishimo ambapo vijana hupiga vijipira kwa miti huku lengo lao likiwa kuweka mipira yote kwa vishimo. Kila mchezaji hujaribu kila awezalo kuhakikisha kwamba yeye ndiye atakayerusha mipira mingi zaidi ndani ya vile vijishimo.

Related Posts