Na Emmanuel Massaka Michuzi TV
MWENYEKITI wa UVCCM Kata ya Mabwepande Andrew Mashimba amesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu ndani ya Chama hakuna kukatwa ambapo mshindi wa kwenda kugombea katika nafasi ya mwenyekiti wa Mtaa na wajumbe watapatikana kwenye boksi la kura.
Viongozi wote watapigiwa kura na wanachama hivyo hakuna mtu atapita Kwa kura za mezani za viongozi kufanya kupendekeza.
Mashimba ameyasema hayo katika mkutano wa Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Mbopo jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kuwa wananchi wajitokeze katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kuanzia Septemba 11 hadi 20 huku wana CCM wajiandikishe ndani ya siku Nne zinatosha na sio kusubiri siku ya mwisho ya kujiandikisha.
Amefafanua kuwa mwenyekiti wa Chama Dkt.Samia Suluhu Hassan ametangaza utaratibu mzuri wa kufanya kila mwanachama ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.