Mwenge wa uhuru wahitimisha kukimbizwa Kagera,wafika kwenye mradi wa KADERES na RUWASA .

Mwenge wa Uhuru umehitimisha mbio zake Mkoani Kagera na kukabidhiwa Mkoani Geita tayari kwa ajili ya kukimbizwa Mkoani humo.

Kwa Mkoa wa Kagera umemalizia katika Wilaya ya Muleba ambapo umekagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa kilimo wa vijana,uzinduzi wa mradi wa maji unaotekelezwa na RUWASA katika kata ya Kishanda ambao unatarajia kupunguza changamoto ya maji kwa asilimia kubwa hususani kwa wakazi wa maeneo ya mradi.

Aidha mwenge wa uhuru ulipita katika kitalu cha miche ya uendelevu wa utunzaji wa mazingira chini ya kampuni ya KADERES peasant development, ambapo miche itakayozalishwa katika hiki na kupandwa kwa wananchi itatumika katika uvunaji wa hewa ya ukaa kupitia mradi wa uvunaji wa hewa ya ukaa.

Akisoma taarifa ya mradi huo Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya KADERES Leodgard Kachebonao amesema kuwa mradi huo umegharimu zaidi ya milioni 500 za kitanzania na unatarajia kunufaisha wananchi wote wenye uhitaji wa miche Wilayani Muleba.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2024 Godfrey Mzava amewapongeza kwa hatua hiyo kubwa ambayo wameamua kuifanya itakayowapa ajira vijana wengi ikiwa ni pamoja na kuwapa utajiri kupitia kilimo.

Related Posts