Wanariadha wa wizara, taasisi waonesha viwango katika SHIMIWI

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Wanariadha wanawake na wanaume wa Wizara, Idara, Wakala na Ofisi za Wakuu wa Mikoa leo wameonesha viwango vya juu kwenye fainali za mbio za mita 100, 200, kupokezana vijiti 4×100, 400, 800, 1,500 na 100 kwa watu wazima wenye umri kuanzia miaka 50, katika michezo ya SHIMIWI inayoendelea mkoani hapa.

Katika fainali za mbio za mita 1,500 wanaume ubingwa umechukuliwa na Paulo Remy wa Ikulu; huku nafasi ya pili ikienda kwa Joseph Kachala wa Wizara ya Afya na mshindi wa tatu ni Deonatus Magendelo wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; katika fainali ya mita 100 kwa wanawake ameshinda Jackline Daniel wa Wizara ya Maji, akifuatiwa na Furaha Kaboneka wa Ukaguzi na watatu ni Pendo Manjale wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kwa upande wa fainali za wanaume za mita 100 ameshinda Baraka Mashauri wa Wizara ya Uchukuzi, akifuatiwa na Paulo Tarimo wa TAKUKURU, na watatu ni Yunusi Mkurukute wa Mahakama; wakati ubingwa wa mbio za mita 100 za watu wazima wenye umri wa miaka 50 umechukuliwa na Shaibu Kanyochote wa Mahakama, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Charles Masanga wa RAS Mara na ushindi wa tatu umekwenda kwa Juma Chikuku wa Wizara ya Kilimo.

Katika fainali za mbio za mita 400 kwa wanawake ubingwa umechukuliwa na Mastura Kaiza wa Wizara ya Uchukuzi, akifuatiwa na Upendo Gustafa wa Mahakama na watatu ni Nyamwiza Ndibalema wa Wizara ya Madini; wakati kwa wanaume ameshinda Pwele Jackson wa Wizara ya Elimu, akifuatiwa na Peter Masinde wa Wizara ya Afya na watatu ni Marire Witimu wa TAKUKURU; wakati bingwa wa mita 1,500 kwa wanawake ni Justa Tibendelana wa Mahakama, akifuatiwa na Martha Kunzugala wa TAKUKURU na Pendo Manjale wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kwa upande wa mita 200 wanaume ameshinda Pwele Jackson wa Wizara ya Elimu, wapili ni Yunusi Mkulukuta wa Mahakama na wa tatu ni Omary Mwenda wa RAS Shinyanga; wakati kwa wanawake ameshinda Mastrura Kaiza wa Wizara ya Uchukuzi, wapili ni Judith Malata wa Ofisi ya Mashtaka ya Taifa na watatu ni Mwajabu Bwire wa Mahakama; wakati bingwa wa mita 800 kwa wanaume ni Salimu Mwangi wa Ofisi ya Rais Ikului, akifuatiwa na Marire Witimu wa TAKUKURU na watatu ni Ramadhani Wakilongo wa Wizara ya Uchukuzi; huku mbio za kupokezana vijiti mabingwa kwa wanaume ni Ikulu, wakifuatiwa na TAKUKURU na watatu nui Wizara ya Uchukuzi; wakati wanawake ni Ikulu, wakifuatiwa na Wizara ya Maji na watatu ni Mahakama.

Katika hatua nyingine timu ya michezo wa netiboli ya Ikulu wametinga nusu fainali kwa kishindo baada ya kuwafunga Wizara ya Elimu kwa maboli 77-38; nayo Hazina waliwachapa Ofisi ya Bunge kwa 44-43; nao Wizara ya Afya waliwaliza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa magoli 71-32 na Wizara ya Ardhi nayo imefuzu kwa hatua ya nusu fainali. Wakati kwa mchezo wa mpira wa miguu Ikulu wamefuzu baada ya kuwafunga Mahakama kwa magoli 4-3; huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wamewashinda Wizara ya Mifugo na Uvuvi,wakati Wizara ya Maji waliwaondosha Wizara ya Afya kwa bao 1-0 na Utumishi wamefuzu baada ya kuwafunga Hazina.

Related Posts