DC LUDEWA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI

Katika kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2020 – 2025 unaendelea kwa ubora na kusimamia vyema, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Olivanus Thomas amewasilisha taarifa ya utekelezaji huo mbele ya wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilayani Ludewa Mkoani Njombe, ambapo miongoni mwa miradi iliyoelezewa ni miradi ya afya na elimu .

Aidha Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema katika sekta ya Maji tayari Kuna fedha ambazo zimetolewa na serikali kwaajili ya utekelezaji wake katika maeneo mbalimbali ikiwemo mradi wa Sh. Bil. 7.5.

Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani humo Stanley Kolimba amesema tangu kupata uhuru Chama hicho kumekuwa imara katika kuleta maendeleo ya wananchi, hivyo amewaasa wananchi kuendelea kukiunga mkono.





Related Posts