Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Nchini Tanzania Shigeki Komatsubara amesema UNCDF imeweza kutoa fedha zaidi ya dola za kimarekani milioni 12 (takriban shilingi bilioni 33 za Tanzania) kwa miradi inayolenga jamii ikiwa ni awamu ya pili ili kupunguza mabadiliko ya tabianchi katika Wilaya za Kondoa, Chamwino na Mpwapwa katika Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar.
“Zaidi ya watu 10,500 katika Mkoa wa Dodoma ambao unakabiliwa na changamoto za ukame wamenufaika moja kwa moja na miradi iliyobainishwa na jamii ili kuwasaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya, Sweden na Norway
Amesema UNCDF ilianza na majaribio kama awamu ya kwanza ili kupima mbinu ya kuelekeza fedha za tabianchi kwa halmashauri chache kabla ya kupanua uwigo na kufikia halmashauri nyingi zaidi katika awamu ya pili ambapo unategemea kukamilika mwaka 2027.
“UNCDF inatarajia kuanza kufanya tathmini ya athari ya mabadiliko ya tabianchi katika ngazi ya wilaya pamoja na Zanzibar ambapo matokeo ya tathmini hii yatasaidia kuandaa mipango katika ngazi ya halmashauri, kata na vijiji ambayo itakuwa inaakisi hali halisi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi.” alisema Komatsubara
Naye Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Bi. Farhat Mbarouk amesema uwekezaji katika miundombinu ya maji, miradi ya kilimo inaweza kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuboresha maisha ya wakulima na juhudi za kulinda Pwani pamoja na uhamasishaji wa jamii na kujenga uwezo katika ngazi ya jamii na serikali za mitaa.
Pia Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Kemilembe Mutasa ameshukuru Shirika la Umoja wa mataifa la Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto za tabianchi katika maeneo mbalilimbali hapa nchini na kusisitiza kuwa serikali iko bega kwa bega na Shirika hilo
UNCDF pamoja na washirika wake inaunga mkono nchi zenye uhitaji katika kukuza uchumi wao, ikiwa ni pamoja na uwezo wao wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia ruzuku, mikopo, na dhamana nchini Tanzania ambapo serikali inatekeleza Mpango wa UNCDF wa wukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (LoCAL), ambao unatumia Ruzuku za Ustahimilivu wa Tabianchi zilizopangwa kwa Utendaji (PBCRGs) kuelekeza fedha kwa serikali za mitaa kwa kutumia mifumo ya uhamasishaji ya kitaifa.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Nchini Tanzania Bw. Shigeki Komatsubara akizungumza kuhusu namna shirika ilo lilivyojipanga kutekeleza awamu ya pili ya mpango wa kuongeza uwezo wa serikali, halmashauri na vijiji kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi hapa nchini.
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Bi. Farhat Mbarouk kizungumza kuhusu Serikali ya Zanzibar ilivyojipanga kushirikiana na Shirika la Umoja wa mataifa la Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) ili kuweza kutekeleza miradi mbalimbali hasa kwa awamu ya pili ya mpango wa kuongeza uwezo wa serikali, halmashauri na vijiji kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Kemilembe Mutasa akielezea ushirikiano wa kati ya Tanzania pamoja na mashirika ya Umoja wa mataifa wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi awamu ya pili ya mpango wa kuongeza uwezo wa serikali , halmashauri na vijiji kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi hapa nchini.
Naibu Mkurugenzi – UNCDF Jenifer Bukokhe Wakhungu akizungumza kuhusu namna shirika hilo lilivyotekeleza mpango wa awamu ya kwanza pamoja na uzinduzi rasmi awamu ya pili ya mpango wa kuongeza uwezo wa serikali , halmashauri na vijiji kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi hapa nchini.
Mratibu wa mradi wa Mabadiliko ya tabianchi wa UNCDF- LoCAL, Aine Mushi akiwasilisha mada kuhusu mradi wa kwanza ulivyotekelezwa wakati wa uzinduzi rasmi awamu ya pili ya mpango wa kuongeza uwezo wa serikali , halmashauri na vijiji kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi hapa nchini
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Nicola Brennan akitoa salamu katika uzinduzi huo
Mwakilishi wa Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Benjamin Sturtewagen akitoa salamu katika uzinduzi huo
Mwakilishi kutoka Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Lamine Diallo akizungumza kuhusu ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na mashirika ya Umoja wa Mataifa hasa Shirika la Umoja wa mataifa la Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)
Afisa Mipango kutoka Halmashauri ya Mpwapwa James Messo akizungumza kuhusu namna walivyoupokea na kuutekeleza mradi katika wilaya ya Mpwapwa
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia mada wakati wa zinduzi rasmi awamu ya pili ya mpango wa kuongeza uwezo wa serikali , halmashauri na vijiji kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi hapa nchini
Uzinduzi rasmi awamu ya pili ya mpango wa kuongeza uwezo wa serikali, halmashauri na vijiji kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi hapa nchini
Picha ya pamoja