Tshabalala: Bado niponipo sana tu

KAMA ulikuwa unawaza nahodha wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ anaweza akatundiga daruga hivi karibuni, basi sikia majibu yake.

Tshabalala amejibu swali aliloulizwa na Mwanaspoti kutokana na kucheza kwa kiwango bora ndani ya misimu 10 katika kikosi cha Simba hawazi kustaafu?

Na haya ndiyo majibu yake: “Sina wazo kabisa la kustaafu kwa sasa. Kikubwa nina nguvu ya kuisaidia timu, basi ninaweza nikacheza miaka mingi, labda itokee nimepata changamoto ya kuniweka nje.”

Tshabalala amesema kinachomfanya asishuke kiwango ni kuzingatia mazoezi, kujituma, usikivu na kuyafanyia kazi yale ambayo anaelekezwa na makocha, lakini kubwa zaidi ni kwamba halewi sifa.

“Siyo kazi rahisi, lakini natambua soka ndio linaloendesha maisha yangu lazima nijitume na kujitunza. Pia siyo mvivu wa kufanya mazoezi kwa bidii,” amesema.

Nje na soka, Tshabalala amesema anapenda sana kufanya kazi ya U-DJ.

“Ndio maana nimuumini wa kuwaangalia DJ’s mbalimbali, kwani nisingefanikiwa katika mpira wa miguu, basi ningefanya kazi hiyo,” akasema.

Related Posts