Na Yeremias Ngerangera – Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed aliwashukuru waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma Kwa kuitangaza vyema ziara ya Raisi alipokuwa Mkoani Ruvuma.
Kanali Ahmed Abbas Ahmed aliwashukuru waandishi wa habari kwenye kikao alichokifanya na waandishi hao ofisini kwake mara baada ya kumalizika Kwa ziara ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkoani humo.
Hata hivyo Kanali Abbas aliwataka waandishi wa habari kushirikiana na ofisi yake ili kuutangaza vyema Mkoa wa Ruvuma .
Pamoja na hayo Kanali Abbas alitumia kikao hicho kuwashukuru wananchi wa Mkoa wa Ruvuma Kwa kujitokeza Kwa Wingi kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan alipokuwa Mkoani Ruvuma .
Ngaiwona Nkondora mwandishi wa habari wa Radio free Afrika Mkoa wa Ruvuma alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kwa kuwaita waandishi wa habari ofisini kwake na kuwashukuru ,kitendo hicho kinawafanya waandishi wa habari Kujua Mkuu wa Mkoa anathamini kazi zinazofanywa na waandishi wa habari katika Mkoa wake alisema Ngaiwona.
Ziara ya Raisi wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan Mkoani Ruvuma ilianza tarehe 23 hadi tarehe 28 mwezi Septemba Mwaka huu ambapo katika Ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aliwashukuru waandishi wa habari wa Mkoa wake Kwa kuchapa kazi nzuri ya kuitangaza ziara ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano Dk Samia Suluhu Hassan.