Katika hali iliyotarajiwa, Iran imeishambulia kwa mabomu Israel usiku wa kuamkia leo Jumatano, Oktoba 2, 2024.
Mashambulio hayo yamefanyika kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Israel na kundi la Hezbollah la Lebanon.
Israel ilianzisha mashambulizi katika mji wa Beirut nchini Lebanon na kusababisha mauaji ya aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo, Hassan Nasrallah.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeshuhudia alama za tahadhari ya mashambulizi ya anga nchini Israeli, ambapo wakazi walihimizwa kukimbilia mafichoni, huku milipuko ikisikika na mifumo ya ulinzi wa anga ikiwekwa.
Mianga ilionekana usiku katika maeneo mbalimbali ya nchi, huku ndege zisizo na rubani na makombora yakidunguliwa na Israeli na washirika wake kabla ya kufika Israeli.
Kuna ripoti kuwa kombora moja la masafa marefu lilidunguliwa nje ya anga ya dunia.
Mbali na Iran, inaelezwa nchi zaidi ya tisa zinahusika katika mzozo huo wa kijeshi, huku makombora yakirushwa kutoka Iran, Iraq, Syria, na Yemen na kudunguliwa na Israeli, Marekani, Uingereza, na Jordan.
Shambulizi hilo lilihusisha ndege zisizo na rubani, makombora ya cruise na makombora ya masafa marefu.
Iran ilirusha zaidi ya ndege zisizo na rubani 300 na makombora kuelekea Israeli, Jeshi la Israeli lilisema Jumapili. Shambulizi hilo lilijumuisha ndege zisizo na rubani 170 na makombora ya cruise 30, ambayo hakuna hata moja lililoingia Israeli, na makombora ya masafa marefu 110, ambapo machache yalifika Israeli.
Jeshi la Mapinduzi la Iran (IRGC) lilisema lilirusha ndege zisizo na rubani na makombora hayo. Vyanzo vya usalama vya Iraq vilisema makombora yalionekana yakipita juu ya Iraq kuelekea Israeli.
Wakati nchi hizo za Kiarabu zikiishambulia Israel, Jeshi la Marekani nalo limesema vikosi vyake vilidungua makombora na ndege zisizo na rubani kadhaa zilizorushwa kutoka Iran, Iraq, Syria, na Yemen.
Jinsi ulinzi wa anga wa Israeli ulivyokabiliana na mashambulizi hayo: Takriban asilimia 99 ya makombora yaliyovurumishwa yalidunguliwa nje ya anga ya Israeli au juu ya anga ya nchi hiyo.
Hii ilijumuisha ndege zote zisizo na rubani na makombora ya cruise. Mfumo wa Arrow ulitumika kuzuia makombora ya masafa marefu, huku Iron Dome ikiingilia kati makombora yasiyolengwa na drones.
Washirika wa Israeli walisaidia pia, huku Marekani ikitua ndege za kivita na meli za kivita kusaidia Israeli kudungua makombora na drones yaliyovurumishwa kutoka Iran. Rais wa Marekani, Joe Biden amesema vikosi vya Marekani vimesaidia kudungua makombora na ndege zisizo na rubani kadhaa.
Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu amewataka Waisraeli kufuata maagizo ya usalama na kusimama pamoja dhidi ya kile alichokiita, ‘mhimili wa uovu’ wa Iran, akisisitiza kwamba nchi itapambana na kushinda vitisho.
Makamu Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya (EU), Josep Borrell amelaani vikali shambulio la makombora la Iran dhidi ya Israeli.
“Mzunguko huu wa hatari wa mashambulizi na kisasi una hatari ukiachwa bila kudhibitiwa. Inahitajika kusitisha mapigano mara moja kwenye eneo hilo,” ameandika katika ujumbe alioyutuma mtandao wa X (zamani Twitter).
Shambulio la Iran lilikuwa mara mbili zaidi ya mashambulizi yake ya Aprili kwa mujibu wa idadi ya makombora ya masafa marefu, kwa mujibu wa makao makuu ya kijeshi ya Marekani (Pentagon).
Katika mkutano na waandishi wa habari, Ofisa habari wa Jeshi la Marekani, Meja Jenerali, Patrick Ryder amesema askari wawili wa Jeshi la Wanamaji la Marekani walifyatua karibu vizuizi kadhaa dhidi ya makombora ya Iran, lakini hakuthibitisha kama walifanikisha kuyadungua makombora hayo.
Wananchi Iran washerehekea
Wakati mashambulio yakiendelea, huko Iran sherehe zilifanyika mitaani Tehran, ambapo watu wengi wamepeperusha bendera za Iran na Hezbollah, na kuonyesha picha za kiongozi wa zamani wa Hezbollah aliyeuawa katika shambulio la anga la Israeli nchini Lebanon.
Marekani, Uingereza waunga mkono Israel
Rais wa Marekani, Joe Biden amesema Marekani inaunga mkono kikamilifu Israeli kufuatia shambulizi la kombora la Iran.
Amesema kwa maagizo yake, jeshi la Marekani limesaidia kikamilifu katika ulinzi wa Israeli wakati wa shambulizi hilo.
Kulingana na taarifa za sasa, Biden amesema shambulio hilo linaonekana limeshindwa na halikufanikiwa.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer amelaani shambulio la Iran dhidi ya Israeli.
Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya Downing Street London, Starer alipokuwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, amesema kuna dhamira thabiti ya Uingereza kusaidia usalama wa Israeli na ulinzi wa raia.
Pia amezungumzia umuhimu wa kusitisha mapigano nchini Lebanon na akaibua hoja hali inayoendelea Gaza.
Aidha, Sir Keir amezungumza na Mfalme Abdullah II wa Jordan, ambapo walitaka kupunguza mvutano ili kuzuia hali mbaya ya kibinadamu.
Waziri Mkuu alisema atashirikiana na washirika wake na kufanya kila awezalo kushinikiza kumaliza mvutano na kutafuta suluhisho la kidiplomasia.
Mabalozi wa Iran, Israel watoa kauli kali
Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani, amehalalisha shambulizi hilo kwa kusema lilikuwa ni hatua ya kujihami baada ya mauaji ya viongozi wa juu wa Hamas na Hezbollah.
Balozi wa Israeli katika Umoja wa Mataifa, Danny Danon, ameahidi kulipiza kisasi mashambulizi hayo akisema itakuwa ni ya kuumiza.
Ameongeza Israeli haina nia ya vita lakini haiwezi kukaa kimya wakati raia wake wanashambuliwa.