Wananchi wa Tabata Kisukuru waiomba Serikali kuwapatia makazi baada ya nyumba zaidi ya 10 kusombwa na maji

Wananchi wa Tabata Kisukuru Banebane mtaa wa Tutu, wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam wameiomba Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan iwasaidie makazi kufatia tukio la kuporomoka kwa Nyumba zaidi ya 10 zilizopakana na njia ya maji ya bonde la mto msimbazi iliyopita Tabata Kisukuru.

Akizungumza leo mbele ya Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa Wananchi wa mtaa wa Tutu, Allen Kahemela ameiomba Serikali iwasaidie makazi kufatia tukio la kuporomoka kwa Nyumba zao sambamba na kuiondoa kona ambayo imewekwa kimakosa kwani imeondoa njia rasmi ya mto na kusababisha kupitia njia isiyo rasmi.

” Tunaiomba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt Samia itusaidie makazi kwani kwa sasa hatuna makazi rasmi zaidi ya kuishi katika maeneo ambayo tumepewa hifadhi na watu wetu wa karibu, tumekuwa na malalamiko haya kwa muda wa miaka 3 sasa lakini bado hatujasaidiwa, tunakuomba Mhe. Rais utusaidie ” Amesema Kahemela.

 

Related Posts