TET YAINGIA MAKUBALIANO NA ENABEL KUBORESHA ELIMU NCHINI

TAASISI ya Elimu ya Tanzania (TET) na Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (ENABEL) wametia saini rasmi hati ya makubaliano kwa ajili ya kuboresha elimu nchini katika maeneo makuu matatu.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba ameyataja maeneo waliyokubaliana ni pamoja na Kuandaa vifaa vya kufundishia na kujifunzia,Kusaidia utekelezaji wa stadi za maisha katika mitaala na Kusaidia katika kutoa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) kwa kutumia mfumo wa ujifunzaji na walimu unaojulikana kama LMS na katika jumuiya za ujifunzaji zinazotekelezwa katika ngazi ya shule, kata au vituo vya ujifunzaji vya walimu yaani TRC

“Tuna uhakika kuwa kwa kuunganisha nguvu, ushirikiano huu utaleta maboresho makubwa katika mfumo wetu wa elimu hapa nchini” amesema Dkt. Komba.

Dkt. Komba ameongeza kwa kusema kuwa maeneo hayo tajwa yanaendana vema na mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2023 ambao umeanza kutumika mwaka 2024.

Ametaja maboresho ya mitaala yaliyofanyika ni pamoja na kuandaa vifaa vya kufundishia, vya kujifunzia, na vya rejea—vitawasaidia wanafunzi kupata maarifa na ujuzi unaohitajika.

Stadi za Maisha ni moja ya masuala mtambuka katika mtaala ulioboreshwa. Kupitia ushirikiano huu, tunalenga kuimarisha utoaji wa elimu ya stadi za maisha kwa kuzichopeka katika ufundishaji wa masomo mbalimbali.

Ameeleza kuwa suala la Mafunzo Endelevu Kazini (MEWAKA) ni jambo linalohakikisha walimu wanakuwa na ubora kwa kupata mafunzo na limezingatiwa katika makubaliano hayo.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkazi wa Enebel,Bw. Koenraad Goekint amesema ni matumaini yao kuwa makuabaliano hayo yatasaidia katika kuinua elimu Tanzania na kushukuru kupata fursa ya kushirikiana na TET katika eneo la elimu kwa ujumla.















Related Posts