MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza mahakama kuwa tangu mwaka 2016 hadi sasa hana mahusiano mazuri na jirani yake Deogratus Minja ndiyo maana amemsingizia kuwa amemjeruhi kwa kumpiga kutokana na hila zake.
Masahi anatuhumiwa Januari 11, 2023 akiwa eneo la Mbezi Msakuzi ndani ya Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam alimpiga Deogratus Minja kwa nyundo na kumsababishia kupata madhara makubwa ya mwili mwake kwa madai kuwa kwanini alikwenda kumshtaki serikali za mtaa kwamba anatililisha maji machafu.
Masahi amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi, Amos Rweikiza wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam wakati akijitetea juu ya mashtaka yanayomkabili ya kumjeruhi Minja huku akiongozwa na Wakili wake, Nestory Wandiba.
Amedai kuwa anamfahamu Minja ndiyo kama jirani yake ambae wamepakana nae kwa ukuta wa uzuio ambao umezingira nyumba yake, ujirani wao ni wa takribani miaka nane, yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuhamia eneo hilo la Mbezi mwaka 2012 na Minja alihamia hapo mwaka 2016.
“Kuna matatizo kama matatu ambayo yamesababisha kutokuwa na mahusiano mazuri, jirani yangu alijenga kibanda cha kuku katika dirasha la chumba changu, halufu ikawa inaingia chumbani na ikaniathiri kiafya,”
“Hivyo nilishirikisha serikali za mitaa, wakaja wakamshauri kujenga ukuta mrefu ili hewa iweze kupita juu isiingie chumbani, alijenga huo ukuta mrefu na kuhamisha kibanda hilo likaisha,”alimedai Masahi.
Aliendelea kudai kuwa, baada hilo kuisha likaja lingine la kugombania mpaka, Minja yeye alinunua eneo dogo, akasema kuna mita nne ambazo ni za kwake baina ya mpaka wake na wangu, yeye akaona mita nne ndiyo nini akaamua kumuachia, badae akajenga nguzo kubwa kuzuia mpaka ambao unatengeneza uchochoro.
“Hilo nalo likaisha, jinamizi likaja tena jirani yangu alichukua zege anaziba tena kwenye mtaro maji niliyoutengeneza mimi ili maji yasipite, yeye binafsi alikwenda serikali za mitaa, walipofika hapo wakukuta maji hayakanyagi wala hayafiki kwake. Hizo ndiyo ishu tata ambazo zilisababisha mahusiano mabovu na jirani yangu,”amedai Masahi
Aliendelea kudai kuwa anakumbuka Januari 11, 2023 alitoka kazini majira ya saa mbili na nusu usiku, akakuta Minja anazozana na shemeji yangu Lipopo Sitini getini kwake, lakini sikujua ni wanini kwa sababu nilikuwa ndani ya gari,nilifunguliwa geti nikaingia ndani nikaendelea na shughuli zangu sikutaka kujua kilichokuwa kinaendelea.
“Baada ya mimi kuingia ndani sikuweza kujua ugomvi uliishaje hadi kesho yake polisi walipokuja kunifuata mida ya saa nane na nusu mchana, wakiieleza kuwa nimemshambulia jirani yangu,”
“Nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni sikukuu ya mapinduzi ya Zanzibar ilikuwa ni siku ya ijumaa, nililipoti kituo cha polisi nikaa mahabusu ijumaa hadi jumapili saa 10 jioni nilipoachiwa, baada ya hapo niliwambiwa niwe naripoti kituoni wakati huo uchunguzi unaendelea,”amedai Masahi
Akijibu masawali ya Wakili wa Serikali, Chesensi Gavyole, Masahi amedai kuwa alikuta shemeji yake akizozana na jirani lakini hakufuatilia kujua nini ambacho kilikuwa kinaendelea baina ya watu hao wawili.
Wakili: Shahidi umeieleza mahakama kuwa ulimkuta shemeji yako akizozana na jirani yako getini kwako.
Shahidi: Ndiyo
Wakili: Baada ya kuona wazozana wewe uliingia ndani ni sahihi
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Naa wewe ni mwenye nyumba
Shahidi: Ndiyo
Wakili: Na huyo alikuwa anazozoana ni shemeji yako
Shahidi: Ndiyo
Wakili: Kwanini hukuona umuhimu
Shahidi: Kwababu nilikuwa na gari mimi nikaingia ndani
Wakili: Kwanini hukutoka tena nje
Shahidi: Kulingana na tabia ya jirani yangu mimi sikutaka kabisa kujiingiza kwenye tafulani hiyo
Wakili: Lakini si unajua wewe ni mwenye nyumba na huyo ni shemeji yako na lolote lingweza kutokea,
Shahidi: Sikuona maana ya kuingilia mzozo wao kwa sababu walikuwa mbali mbali
Wakili: Baada ya kuingia ndani hukutoa taarifa popote kutokana na huo mzozo na jirani yako
Shahidi: Sikutoa taarifa popote
Wakili: Na ulikamtwa lini
Shahidi: Januari 12, 2023
Wakili: Baada ya kufikishwa kituo cha polisi ulielezwa ni tuhuma gani
Shahidi: Walivyofika askari na mjumbe nyumbani kwangu walinieleza kwamba nimemshambulia jirani yangu Januari 11,2023 saa mbili na nusu usiku
Wakili: Kwa muda huo ulikuwa wapi
Shahidi: Ni kama nilivyoeleza mahakama kuwa nilikuwa kazini.
Wakili: Kwa hiyo ulikuwa nyumbani kwako
Shahidi: Ndiyo
Wakili: Nani aliyemshambulia jirani yako
Shahidi: Hadi sasa hata sijui, kutokana na ugomvi wetu
Wakili: Wewe ulichukuliwa maelezo polisi , ulisema nani alimshambulia jirani yako
Shahidi: Nilikana polisi kuwa sikumshambulia
Wakili: Kwanini umeshtakiwa wewe
Shahidi: Kama nilivyoeleza nimeingizwa kwenye huu ugomvi kutokana na uhasama ambao ninao na jirani yangu
Wakili: Je uliwaweleza polisi kuwa ulimkuta shemeji yako akizozana na jirani yako?
Shahidi: Sikuwaeleza
Wakili: Kwa nini hukuona umuhimu wankufanya hivyo
Shahidi: Kwa sababu ni jukumu la polisi kumtamfuta mtenda wa hilo kosa.
Wakili: Shemaji yako wakati unakamtwa alikuwa wapi
Shahidi: Alikuwepo nyumbani
Wakili: Polisi wangejuaje kama ni shemeji yako kama wewe usingewaambia kuwa shemeji yako na jirani walikuwa na mzozo
Shahidi: Mtu sahihi aliyetakiwa kujibu mashtaka hayo ni shemeji yangu
Wakili: Kwanini hukuwaeleza polisi
Shahidi: Sikuona sababu ya kuwaeleza polisi kwa sababu hawakuniuliza
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 30, 2024 kwa jili ya kutolewa hukumu.