TOC WAMSHUKURU MKUFUNZI WA JUDO KUTOKA UTURUKI


Na Khadija Kalili Michuzi Tv
KAMATI  ya Olimpiki Tanzania (TOC) imeipongeza nchi ya Uturuki kwa kuwapatia Mkufunzi aliyetoa mafunzo kwa walimu wa mchezo wa Judo nchini.
Makamu wa Rais (TOC) Henry Tandau amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya walimu wa mchezo huo yaliyofanyika kwenye shule ya Filbert Bayi.
Tandau amesema kuwa mafunzo hayo yameendeshwa na mkufunzi mwenye uwezo mkubwa na kuwapati mbinu nzuri walimu wa mchezo huo.
Kwa upande wake Katibu wa (TOC) Filbert Bayi amesema kuwa walimu hao wazingatie mafunzo hayo ili kuendeleza mchezo huo kupitia mashuleni.
Rais wa chama cha Judo nchini (JATA) Zaidi Omary amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa mchezo wa judo.
Akisoma risala ya washiriki wa mafunzo hayo Geophrey Mtawa amesema kuwa wanaiomba serikali kuwapatia magodoro na mafunzo ya mara kwa mara.
Mafunzo hayo ya siku 10 yamesherikisha walimu 24 wa mchezo wa Judo kutoka Bara na Visiwani.

Related Posts