Waziri Gwajima kukabidhi nyumba kwa mjane aliyefukuzwa baada ya kugoma kurithiwa.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum, Doroth Gwajima anatarajia kukabidhi nyumba kwa mjane Judith Innocent Luhumbika, aliyekuwa akipitia manyanyaso kutoka Kwa familia ya ndugu wa mumewe, ikiwemo kufukuzwa nyumbani kwake kufuatia kugoma kurithiwa mara baada ya mumewe kufariki.

Akizungumza katika nyumba hiyo yenye thamani ya zaidi ya milioni 50, aliyojengewa kwa msaada wa wadau mbalimbali Kwa kushirikiana na taasisi ya GH Foundation chini ya Mkurugenzi wake Godlisten Malisa, Judith amesema alikuwa akilala katika Stendi ya Mabasi ya zamani Ubungo na Watoto wake Watano bila kukosa msaada Kwa zaidi ya miezi minee na baadaye alipata msaada wa kuangiwa chumba na kusomeshewa Watoto.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano wa GH foundation James Mbowe amesema nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Makondeni, Kata ya Msongora, Chanika Mvuti Wilayani Ilala Jiji Dar es Salaam, itakayokabidhiwa siku ya Jumapili ya Mei 5, 2025 ni ya nne tangu kuanza kutoa misaada kwa wenye uhitaji, huku akiwataka watanzania kuacha tabia za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya Wanawake na kupelekea kuwakosesha haki zao za msingi.

default

 

Related Posts