MBEGU ZA MITI YA ASILI KUONGEZA UHIFADHI ENDELEVU

 

Wataalamu na taasisi zinazohusika na utoaji wa taaluma na utafiti wa Misitu wametakiwa kutumia taaluma zao kufanya tafiti zitakazo saidia kuishawishi Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha ‘stoo’ ya mbegu ya muda mrefu (Genebank) ya miti ya asili ili kuepuka na kukabiliana na hatari za kupoteza vizazi vya miti ya asili na mimea pori  kutokana na uharibifu wa misitu ya asili na matumizi yasio endelevu ya mazao ya misitu unaoendelea kutokana na shughuli mbalimbali. 

Akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa kwenye mjadala katika maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Kitivo Cha Mafunzo ya Misitu katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi na Meneja Sehemu ya Biolojia ya Mbegu za Miti ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Fandey H. Mashimba amesema kwa sasa kasi ya uharibifu wa misitu inahatarisha vizazi vya miti ya asili kutoweka. “Hali ya baadhi ya mimea ipatayo 314 iliyo katika hatari orodha ya miti iliyo katika hatari ya kupotea duniani kwa mujibu Shirika la Uhifadhi la Kimataifa (IUCN) inaonyesha uhatari unaongezeka unaoweza kutowesha (extinct ) kabisa mimea hiyo kama hakuta kuwa na juhudi mahsusi yaani _species specific conservation action plans_, za kuihifadhi mimea hiyo” , amesema.  Hivyo ipo haja ya wana taaluma wa SUA na wadau wa utafiti kushawishi mamlaka  ili zione haja kama Taifa kuandaa sehemu ya kuhifadhi mbegu za miti na mimea ya asili kwa matumizi ya sasa na vizazi ikiwa kama mimea hiyo itatoweka kwenye maeneo yake ya asili. Nchi nyingi duniani, zinaanzisha stoo za kuhifadhi mbegu muda mrefu (Genebank) akitolea mfano wa nchi ya Uingereza ambayo inayo hifadhi ya mbegu za miti na mimea yote inayopatikan nchini humo kupitia taasisi ya Millenium Seed Bank Partnership .

“Ni dhahiri kuwa kila kukicha misitu ya asili inazidi kuteketea kutokana na shughuli za kibinadamu ambapo kwa mwaka  mmoja takribani hekari 476,000 hupotea. Amesema, mfano kwa sasa miti ya mbao aina ya  Mvule, Mninga na Mkangazi upatikanaji wa mazao yake na mbegu umekuwa ukipungua mwaka hadi mwaka na kuna hatari kubwa baada ya miaka mingine 50 watakao kuwepo wakati huo watakaoshiriki Jubilei ya miaka 100 ya kuanzishwa kwa Kitivo Cha Mafunzo ya Misitu katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, huenda wakapewa tasrifa kuwa miti hiyo imepotea kabisa. Hii ni baadhi tu ya miti michache lakini kuna miti mingine mingi ipo kwenye upungufu mkubwa.  “Hifadhi ya mbegu ya muda mrefu yaani Genebank inaweza ikawa suluhusho la kudunu katika kuhifadhi vizazi vya miti hiyo pamoja na mingine” Mashimba alisema.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa uthibiti wa uagizaji na matumizi ya mbegu za miti kutoka nje ya nchi kwa kuwa unaleta hatari ya kusambaza magonjwa ya miti katika mashamba ya miti ya Serikari na kwenye misitu kwa ujumla. Amesema,  Sheria ya mbegu iliyopo imetaja kuthibiti mbegu za Kilimo. Kutoka na ombwe hilo baadhi ya watu binafsi na kampuni wamekuwa wakitumia mapungufu hayo kuingiza nchini mbegu zisizo hakikiwa na hivyo kuleta hatari ya uinzwaji wa maginjwa ya miti bila Serikari kujua. Sheria ya Misitu haikuainisha uthibiti wa matumizi wa mbegu za miti hivyo kuna ombwe kubwa ambalo lina hatarisha usalama na afya ya sekta ya misitu kama hakutakuwa na uamuzi wa kudhibiti pia matumizi ya mbegu za miti nchini. Hii inajumuisha pia uingizwaji na matumizi ya mimea vamizi katika sekta ya misitu akitolea mfano mti ambao ni maarufu na unaopandwa kwa wingi nchini, muaradi (Mutingia calabura). Amesema tayari mmea huu umeanza kuleta athari jijini Dar es Salaam kwa kuongezeka kwa popo ambao wanatumia matunda ya mti huo kama chakula. 

Ameongeza, uaandaaji wa mipango ya uhifadhi wa misitu yaani Management plans ambao kwa sasa unazingatia uhifadhi jumuishi (Landscape management) ujipambanue zaidi na kubadirika kuweza kutengeneza mikakati ya uhifadhi hadi kwa spishi (Species specific Conservation Action Plans) ambapo kwa sasa watafiti bado hawaoni umuhimu wa kufanya hivyo. Ametoa mfano kwenye sekta ya wanyama pori, mikakati ya uhifadhi imeenda hadi kwenye usawa wa spishi (species level). Ameshauri wana taaluma kuboresha mitaala ya uhifadhi ya misitu kama ilivyo alivyo fafanua kwenye eneo la wanayamapori. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mstaafu wa Misitu na Nyuki Dkt. Fecian Kilahama akitoa uzoefu wake kwenye sekta ya misitu ili kuilwe na tija ya uhifadhi amesema ni muhimu ushauri wa wataalamu wa misitu kuwekewa manani na kuheshimiwa hasa na wanasiasa ili utekelezaji wa sera na sheria ya Misitu uendanane na mahitaji ya sasa katika mabadiliko ya tabianchi na kulinda weledi.

Dkt. Kilahama ameongeza kuwa misitu ya asili ni misitu wezeshi kwenye sekta nyingine na kwamba baadhi ya mambo mengi yanayohusu misitu yanakwama kutokana na mifumo inayogandamiza uhifadhi. Ameshangaa kuona misitu ambayo ni vyanzo vya maji hasa misitu ya Tao la Mashariki inatiririsha maji kwenye mito takribani 90 inayopatikana Tanzania lakini mapato ya matumizi ya maji hayarudi kwenye misitu ili kuongeza uhifadhi. Ameongeza kwa kusema “Natamani itokee siku moja mito yote inayo tiririsha maji kutoka kwenye misitu iache kutoa maji hata kwa siku moja ili watu waone namna misitu inavyochangia uhai na upatikanaji wa maji mijini ndipo labda watajua kwa nini tunataka mapato yatokanayo na matumizi ya maji kwa sehemu yarudi kwenyw uhifadhi”, amesema.

Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa kitivo cha mafunzo ya misitu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wamesema maadhimisho hayo yamekuwa na tija kwani yamewaongezea uelewa wa namna ya kutunza misitu hasa ya misitu ya asili.

Related Posts