Mtangazaji wa Kipindi cha Mashamsham cha WasafiFM Khadija Shaibu maarufu kama Didah, amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa.
Didah ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 42, kifo chake kimetokea siku kumi na sita (16) toka Wafuasi wake washuhudie ukimya wake katika mitandao ya kijamii ambapo chapisho lake la mwisho mtandaoni lilikuwa September 19 2024 ambapo aliweka picha yake akiwa kwenye gari ikisindikizwa na wimbo wa Martha Mwaipaja “amenitengeneza’.