Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Hungary nchini, mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo Dkt. Nchemba ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Hungary kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali watakayoona yanawafaa kutokana na Serikali kuweka mazingira bora yanayovutia uwekezaji. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa kikao chake na Balozi wa Hungary nchini, mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros (Hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadili masuala mtambuka yaliyolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Balozi wa Hungary nchini, mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros, kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo Dkt. Nchemba ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Hungary kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali watakayoona yanawafaa kutokana na Serikali kuweka mazingira bora yanayovutia uwekezaji. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Balozi wa Hungary nchini, mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros, akizungumza wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo Balozi huyo ameahidi kuwa nchi yake iko tayari kusaidia juhudi za Serikali katika kukuza uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi ya huduma za jamii hususan sekta ya maji. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wapili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa kwanza kushoto), Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade (katikati), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise (wa pili kulia), na Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Jabir Selemani (wa kwanza kulia) wakifuatilia kwa umakini mazungumzo ya Balozi wa Hungary nchini, mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba wakifuatilia kwa umakini mazungumzo ya Balozi wa Hungary nchini, mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros (hayupo pichani), aliyefika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kukutana na kuzungumza na Mhe. Dkt. Nchemba, ambapo walijadiliana masuala kadhaa ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Hungary.
Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade (kushoto), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise (katikati), na Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Jabir Selemani (kulia) wakinukuu mambo muhimu yaliyojadiliwa kati ya Mhe. Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) na mgeni wake, Balozi wa Hungary nchini, mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)