DKT. NCHEMBA ATETA NA BALOZI WA HUNGARY

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Hungary nchini, mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo Dkt. Nchemba ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Hungary kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali watakayoona yanawafaa kutokana na Serikali kuweka mazingira bora yanayovutia uwekezaji. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa kikao chake na Balozi wa Hungary nchini, mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros (Hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadili masuala mtambuka yaliyolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.

Balozi wa Hungary nchini, mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros, akizungumza wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo Balozi huyo ameahidi kuwa nchi yake iko tayari kusaidia juhudi za Serikali katika kukuza uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi ya huduma za jamii hususan sekta ya maji. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wapili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa kwanza kushoto), Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade (katikati), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise (wa pili kulia), na Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Jabir Selemani (wa kwanza kulia) wakifuatilia kwa umakini mazungumzo ya Balozi wa Hungary nchini, mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba wakifuatilia kwa umakini mazungumzo ya Balozi wa Hungary nchini, mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros (hayupo pichani), aliyefika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kukutana na kuzungumza na Mhe. Dkt. Nchemba, ambapo walijadiliana masuala kadhaa ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Hungary.

Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade (kushoto), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise (katikati), na Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Jabir Selemani (kulia) wakinukuu mambo muhimu yaliyojadiliwa kati ya Mhe. Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) na mgeni wake, Balozi wa Hungary nchini, mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

BALOZI wa Hungary hapa nchini mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros, ameipongeza Tanzania kwa kusimamia vema sera zake za fedha na uchumi, hatua iliyoifanya iendelee kuimarika kiuchumi na kuahidi kuwa nchi yake itaongeza ushirikiano kwa faida ya nchi hizo mbili.

Mhe. Mészáros ameyasema hayo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa nchi yake imekuwa ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania ikiwemo hatua kubwa inazochukua kuvutia uwekezaji wakiwemo wanaotoka nchini mwake.

Aliahidi kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuchangia maendeleo yake hususan katika sekta za huduma za jamii kama vile maji kupitia mpango wake maalumu wa kushirikiana na Serikali ujulikanao kama Tied Aid Facility.

Akizungumza na Baolozi huyo wa Hungary, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema kuwa uchumi wa Tanzania umeimarika ambapo katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha, uchumi umekua kwa wastani wa asilimia 5.6 ikilinganishwa na ukuaji wa wastani wa asilimia 5 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Alisema kuwa makadirio ya ukuaji wa uchumi katika kipindi cha mwaka 2024/2025 ni wastani wa asilimia 5.4 na asilimia 5.8 mtawalia, kufuatia miongozo na usimamizi mzuri wa uchumi, wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwezi Agosti mwaka 2024, zinaonesha kuwa uchumi wetu umeimarika licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali huku ukuaji huo ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na sekta za ujenzi, kilimo, fedha na sekta ya bima” alisema Dkt. Nchemba.

Aidha, Dkt. Nchemba amemweleza Balozi huyo kuwa kasi ya mfumuko wa bei imedhibitiwa na kuwa katika kiwango cha asilimia 3.1 na kuwa katika wigo wa tarakimu moja, kiwango kilichokubaliwa pia katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilizoweka ukomo wa asilimia 8 na kiwango cha nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) cha asilimia 3 hadi 7.

Amesema kuwa uimara wa uchumi wa Tanzania umethibitishwa pia na mashirika yanayofanya tathimni ya hali ya uchumi wa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Taasisi ya Moody’s ambayo hivi karibuni, iliipandisha Daraja Tanzania kutoka Daraja B2 kwenda Daraja B1 pamoja na Taasisi ya Fitch ambayo imeipa Tanzania Daraja la B+ yenye Mtazamo Chanya (positive Outlook).

Dkt. Nchemba amesema kuwa hatua hiyo imeifanya Tanzania na sekta binafsi kuaminiwa zaidi na taasisi za fedha za kimataifa kwamba zinaweza kuyafikia masoko ya fedha ya kimataifa na kuvutia uwekezaji wa mitaji na teknolojia kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Alitoa wito kwa wawekezaji kutoka Hungary kuja kuwekeza nchini katika maeneo balimbali watakayoona yanawafaa kutokana na Serikali kuweka mazingira bora yanayovutia uwekezaji.

Related Posts