BONIFACE Jacob kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameibuka mshindi kwa nafasi ya Mwenyekiti kanda ya Pwani mara baada ya kupata kura 60 sawa na 77%. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Boni ambaye ameshinda nafasi hiyo huku akiwa mahabusi akikabiliwa na kesi, inayoendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kukosa dhamana mara mbili toka alipofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza tarehe 19 Septemba 2024.
Kada huyo amefanikiwa kushinda uchaguzi huo, mara baada ya kumshinda Gervas Lyenda aliyepata kura 17 sawa na 23%.
Kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti
Ally Mohammed Kadogoo amefanikiwa kuibuka kinara kufuatia kupata kura 51 sawa na 66%.