Bendera ya Tanzania imepeperushwa vyema baada ya Bondia mwenye nyota tatu Mtanzania Ibrahim Mafia, kumchapa mpinzani wake mwenye nyota mbili kutoka Ghana Enoch Tetty Tetteh, kwenye pambano na raundi kumi la kupigania mkanda wa WBC AFRICA BELT.
Enoch amekubali yaishe baada ya kushindwa kuendelea na pambano katika raundi ya 9 na Ibrahim Mafia kuibuka na ushindi wa Technical knockout (TKO) ambapo kutokana na ushindi huo Mafia ameondoka na Knockout ya mama ya shilingi milioni saba.
#KnockoutyaMAMA