Mahamaka yampa Dhamana ‘Boniface Jackob

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachilia huru kwa dhamana aliyekuwa Meya wa Kinondoni na Ubongo jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob ‘Boni Yai’ baada ya kutupilia mbali pingamizi la upande wa Jamuhuri la kuzuia dhamana dhidi yake.

Uamuzi huo umetolewa leo Oktoba 7,2024 na

Hakimu Mkazi Mfawidhi Franco Kiswaga wa mahakama hiyo, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya uamuzi wa kama mshtakiwa apatiwe dhamana au la.

Akisoma uamuzi huo Hakimu Kiswaga amesema kuwa kiapo cha Mkuu wa upelelezi Mkoa (RCO) wa Mkoa wa Polisi Kinondoni Davis Msangi hakina maelezo ya kutosha kuzuia mshtakiwa asipate dhamana hiyo.

Amesemaa, maelezo yaliyotolewa hayana maelezo ya ziada ya kwanini mahakama isitoe dhamana. Iwapo mjibu maombi ametoa maelezo juu ya usalama wake nilitegemea muombaji (Jamhuri) ataleta uthibitisho juu ya maelezo ya Mjibu maombi.

Pamoja na kwamba upande wa majibu maombi haujaleta kiapo kinzani lakini kiapo cha muombaji hakitoshi mahakama kumnyima dhamana mtuhumiwa ukizingatia hii ni haki ya kikatiba .

Mahakama hii haikubali maombi ya Jamhuri hivyo basi mjibu maombi amepewa dhamana kwa masharti ya kuleta wadhamini wa wawili wenye barua za serikali ya mtaa ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh. Milioni saba na pia haruhusiwi kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama.

Jackob amepatadhamana baada ya kusota rumande kwa takribani siku 19 ambapo alifikishwa mahakamani kwa mara ya Septemba 19,2024 akikabiliwa na tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtando wake wa X zamani Twitter.

Katika kesi hiyo Boni Yai anakabiliwa na mashtaka mawili, ya kuchapisha taarifa za uwongo katika mfumo wa kompyuta katika akaunti ya X yenye jina la Boniface Jacob @Ex MayorUbungo kwa nia ya kupotosha umma kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandano namba 14 ya mwaka 2015.

Katika shtaka la kwanza Wakili Manja alidai kuwa , Septemba 12 2024 jijini Dar alichapisha taarifa za uwongo zikimhusisha Mkuu wa Upelelezi wa Kanda (ZCO) ya Dar Es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP).

” Mafwele anatuhumiwa na familia nyingi kama mtu ambaye ameshiriki mauaji kwa moja katika kuwapoteza ndugu wa baadhi ya familia zao, kupotea kwa mfanyabiashara Mussa Mziba, kupotea kwa Deo Mugasa, kupotea kwa Adinani Hussein Mbezi, kupotea kwa vijana watano wa Aggrey” .

Katika shtaka la pilia Wakili Manja alidai kuwa Boni Yai alitenda kosa hilo Septemba 14, 2024 jijini Dar es Salaam akidaiwa kuchapisha taarifa za uwongo kuwa zinazowahusisha Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na utekaji na mauaji ya watu na kutupa miili yao.

Ujumbe huo unasomeka “mkawasifia Ma-RCO (Wakuu wa Upelelezi Mikoa) wanaozuia uhalifu kwa kutenda uhalifu …, bali Ma-RCO waliokuwa kuteka, kukamata, kupiga watuhumiwa risasi, kuwafunga tape, kuwafunga mifuko ya nailoni usoni na kisha kutupa miili ya watuhumiwa ndio wanaijua kazi ya upolisi,”

Related Posts