DC KASILDA AWATAKA WAANDISHI WA DAFTARI LA MKAZI KUFANYA KWA WELEDI NA UFANISI..

NA WILLIUM PAUL, SAME. 

MKUU wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewataka waandishi wa daftari la mkazi kufanya kazi hiyo kwa Ufanisi, udilifu, Usawa na kuhakikisha haki inatendeka, kila mtu mwenye sifa za kuandikishwa aandikishwe ili aweze kupiga kura Novemba 27 mwaka huu. 

Kasilda amezungumza hayo wakati akifungua mafunzo kwa Waandishi wa Daftari la mkazi ambao wanatarajiwa kuanza kazi hiyo tarehe 11 hadi 20 Octoba mwaka huu kwenye Vijiji 100 na Vitongoji 503 vilivyopo Wilaya ya Same.

“Kwenye zoezi hili 2024 tunategemea sana ufanisi wenu ili Wananchi waweze kuitumia haki yao ya msingi ya kuweza kujiandikisha lakini pia kupiga kura Novemba 27 mwaka huu”. Alisema Kasilda.

Aidha katika kikao hicho Waandishi hao wamekula kiapo cha Uadilifu ikiwa ni ishara ya kuwa tayari kuifanya kazi muhimu kwa Taifa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizotolewa na Wizara ya TAMISEMI kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.


Related Posts