ZAINA FOUNDATION, PARADIGM INITIATIVES YATOA MAFUNZO KUHUSU SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TAASISI ya Zaina Foundation kwa kushirikiana na taasisi ya Amnesty pamoja na Paradigm Initiatives zimefanya warsha ya pamoja ambayo imelenga kukuza uelewa wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ambapo itasaidia kuwatetea na kulinda faragha za watu

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 08,2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji Zaina Foundation Bi.Zaituni Njovu amesema Jamii ya watanzania inapaswa kuifahamu sheria hiyo ya ulinzi wa taarifa binafsi na kuwasaidia ili wawe na ulinzi wa faragha zao katika sehemu mbalimbali zinapokuwa zinatumika.

Aidha Zaituni ameeleza kuwa muungano wao katika zoezi hilo umelenga kuwafikia wanawake zaidi ya Elfu10 katika maeneo ya mjini pamoja na pembezoni bila kuwaacha nyuma wanawake wenye changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Mambo ya sera na Sheria,taasisi ya Zaina,Bw. Benjamin Kahale amesema kutokana na Maendeleo makubwa nchini uamepelekea kusababisha kuhitajika kwa Taarifa za watu binafsi ambapo zinatumika kwa uzuri na kwa ubaya.

“Lakini kumekuwepo na taratibu wengine kuvunja taarifa za haki za watu binafsi kwa kutumia taarifa hizo kinyume na matakwa ambayo yamekusudiwa,kwa kupata faida au kwa kuumiza wengine”Amesema.

Vilevile, Mkurugenzi Mtendaji you wa Shirika la Youth and Environmental Justice and Gender Equality (YOGE), Philomena Mwalongo amesema Sheria hiyo ya ulinzi wa taarifa binafsi unahakikisha usalama wa mwananchi pamoja na kumpatia haki zote alizopewa kikatiba.

Pamoja na hayo Philomena amesema kabla ya kutungwa kwa Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi,ulinzi wa taarifa hizo ulikuwepo kwa uhafifu tofauti na wakati huu ambapo sheria ipo na inaelekeza namna ya kufanya endapo atabaini taarifa zake kuvunjwa..

Nae, Mtumishi wa shirika la Paradigm Initiatives,Miriam Wanjiro amepongeza juhudi za serikali ya Tanzania kwa kutunga sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ambapo itawasadia watu kulinda faragha zao.

“Kule Nigeria tulisaidia. mdada ambaye benki ilitumia taarifa zake kufungua aakaunti bila idhini yake,kulingana na sheria za nchi. hiyo haifai,tukaenda mahakamani tukashinda hiyo. kesi”Amesema.













Related Posts