WAZIRI JAFO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPANI NCHINI TANZANIA

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japani nchini Tanzania, Mhe. Yashushi Misawa na Ujumbe wake katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam Oktoba 8, 2024.

Mazungumzo hayo yamelenga kuongeza ushirikiano wa Kibiashara hasa katika Biashara za Viwanda vidogo pamoja na kubadilishana Elimu na Teknolojia na kuendelea kushirikiana kulinda viwanda vilivyoanzishwa miaka ya nyuma. Mfano, Kiwanda cha Redio za Panasonic chenye zaidi ya miaka 55 tangu kuanzishwa kwake.


Aidha, Japani inafanya Biashara za magari aina ya Toyota na vipuli vyake kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania.

Related Posts