Wanafunzi 588 kunufaika na ‘Samia Scholarship’

Jumla ya wanafunzi 588 wa shahada ya awali wamenufaika na fursa za ‘Samia Scholarships’ kwa mwaka huu 2024/2025, ambao wamepangiwa ruzuku yenye thamani ya TZS 2.9 bilioni.

Wanafunzi hawa ni wenye ufaulu wa juu katika tahasusi za sayansi na waliodahiliwa katika vyuo mbalimbali kwenye fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Sayansi za Tiba.

HESLB inawakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku wenye sifa kwa mwaka 2024/2025 ambao bado hawajapangiwa mikopo au ruzuku, kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia ‘SIPA’ wakati taratibu za uchambuzi na upangaji wa mikopo na ruzuku zikiendelea.

Related Posts