WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI UANDIKISHAJI MPAPURA

Na Mwandishi wetu Mpapura

Wananchi mbalimbali wamejitokeza kwa wingi siku ya kwanza ya uandikishaji wapiga kura uchaguzi wa Serikali za mitaa na Vijiji.

“Sisi Wananchi wa Tarafa ya Mpapura tumehamasishwa sana ndio maana tumejitokeza kwa wingi kujiandikisha. Lakini pia maendeleo tuliyoletewa na Serikali yametuhamasisha tujiandikishe ili tukapige kura ya kuchagua viongozi bora watakao endelea kutuletea maendeleo.” Alisema Zuwena Mbele, Mwananchi aliyejitokeza kujiandikisha.

Nae Afisa Tarafa Mpapura Emmanuel Shilatu alipotafutwa alikiri hamasa ipo na Usalama upo pia wa kutosha.

“Kwa taarifa nilizozipata kwa maeneo mbalimbali, na pia maeneo baadhi niliyopita kwa mbali kujionea nimeona wingi wa Watu waliojitokeza kujiandikisha lakini pia wanaendelea kudumisha amani na utulivu. Nawapongeza Wananchi wote wa Tarafa ya Mpapura na ninazidi kuwasisitiza waendelee kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kuanzia sasa tarehe 11-20/10/2024 na wajitokeza kupiga kura kuwachagua viongozi wa Vijiji na vitongozi.” Alisema Gavana Shilatu

Related Posts