DC MPOGOLO AONGOZA WAKAZI WA ILALA KATIKA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA

Na Humphrey Shao

 Mkuu wa Wilaya Ilala Edward  Mpogolo  leo emeongoza wakazi wa Wilaya hiyo katika zoezi la uandikishaji  katika Daftari la Makazi kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unataraji kufanyika Novemba 27, 2024..

Mara baada ya Kujiandikisha DC Mpogolo  alipata furs ya kutembelea Vito vingine Luna hali YA zoezi hilo ambapo  ametembelea Vituo vya Ilala, Upanga na Buguruni

Aidha DC Mpogolo  ametoa wito kwa wakazi wa Ilala kujitokeza kujiandikisha mapema  na kuacha kusubiri mwishoni na hili wajipange katika foleni na misululu ya muda mrefu.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI ) Mhe. Mohamed Mchengerwa aliutangazia  Umma wa Tanzania na Vyama vya siasa kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara utafanyika tarehe 27 Novemba, 2024

Waziri Mchengerwa alieleza hayo leo tarehe 15 Agosti, 2024 wakati akitoa Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuzindua  nembo rasmi  ya uchagunzi wenye kaulimbiu isemayo ” Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki “.

“Ninautangazia Umma wa Watanzania na Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajiri wa kudumu kuwa tarehe 27 Novemba, 2024 itakuwa siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara, Upigaji wa kura utaanza saa mbili kamili za Hasubuhi nakukamilika saa kumi kamili za jioni” alisema mchengerwa.

Related Posts