Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewathibitishia wananchi mazingira ya kujiandikisha, kupiga kura, kuhesabu kura pamoja na kutangaza matokeo kwa Mshindi yatakuwa huru na haki.
RC Chalamila amesema hayo wakati akishiriki zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la wakaazi Katika Kituo Cha Serikali ya Mtaa wa Masaki, amesema amekwenda kujiandikisha Ili awe wapiga kura halali wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu.
Amesema Kama watakumbuka mwaka 2019 wakati Uchaguzi huo kwa mara mwisho kufanyika baadhi ya vyama vya siasa viligomea Uchaguzi na vyama vingine vilifanya Uchaguzi pasipo na vyama vya upinzani na Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kutambua hilo aliamua kuja na 4R ambazo ndani yake kuna masuala maridhiano ambao wote wanahamasishwa kuangalia linaloashiria uvunjifu wa Demokrasia wapaze sauti.
Aidha akizungumzia kuhusu maandalizi ya zoezi hilo, RC Chalamila amesema yako vizuri na ukizingatia Mkoa wa Dar es salaam ndio Mkoa wenyewe idadi ya kubwa ya watu ambao ni zaidi ya Milioni 5.
Hata hivyo RC Chalamila amebainisha kuwa alisikia baadhi ya vyama vya siasa vikilalamika mchakato wa uhamasishaji haujawa huru na haki, huki akisema anaomba wasikie kwa Sababu mchakato huo ufanywa na kila mwenye taarifa na sio vinginevyo
Pamoja na hayo ametoa wito kwa wananchi ujitokeza kujiandikisha Katika Daftari la mkazi ambapo watakuwa wamepata tiketi halali kwa uchaguzi Uchaguzi huo ndio muhimu na unaowahusu wananchi kwa Sababu ya kuwapata Wenyeviti ambao ndio watatuzi wa kero zao.
Chalamila amesema Viongozi wa Serikali za Mitaa ndio walinzi wa wananchi, ndio Viongozi wanaofanya maamuzi na Kamati zao na watu wanaokaa na watu wa chini na kuwasilisha mambo ya wananchi ngazi za juu.
Mbali na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam viongozi wengine waliojiandikisha leo ni pamoja na katibu Tawala wa mkoa huo Dk Toba Nguvila ambaye alipata kujiandikisha katika kituo cha Shule ya Msingi Osterbay.