Ulinzi na usalama waimarishwa zoezi la kujiandikisha Mvomero

Hali ya ulinzi na Usalama katika wilaya ya Mvomero imeimarishwa jambo ambalo limechochea Watu kujitokeza Kwa wingi Kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kwenye vituo mbalimbali katika eneo

hilo.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza Katika Kituo cha kuandikishwa kupiga kura cha Kanisani Kijiji cha Sokoine Mkuu wa Wilaya hiyo Judith Ngulli amesema hamasa iliyofanyika imesaidia watu kujitokeza katika zoezi hilo

Dc NGulli amesema licha ya Leo kuwa Siku ya kwanza ya uandikishaji lakini watu wengi wameonekana kujitokeza katika zoezi hilo ikiwemo akina mama jamii ya kifugaji .

DC Nguli amesema serikali inafuatilia Kwa karibu zoezi hili na hakuna mtu atayevuruga zoezi hilo kwa namna yoyote Ile .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmy ya Wilaya Mvomero Yusuph Makunja amewataka vijana kujitokeza kwa wingi Ili kutumia haki Yao ya kikatiba.

Amesema maendeleo yanaanzia Ngazi ya mtaa na kitongoji hivyo uchaguzi huu muhimu Kwani unatoa fursa kuchagua viongozi ambao ndio wasimamizi wa miradi ya maendeleo.

Naye mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Van Zelland amesema zoezi hilo ni la kiserikali sio la kichama hivyo vyama vyote vinatakiwa kushiriki kutoa elimu.

Zoezi la kujiandikisha katika orodha ua mpiga kura imenza rasmi Octoba 11 mwaka huu hadi octoba 20 ikiwa ni maandalizi ya uchaguguzi wa Serikali za mitaa utakao fanyika novemba 27 mwaka huu.

 

Related Posts