WANANCHI WAENDELEA KUPATA ELIMU KATIKA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA MAAFA DUNIANI OKTOBA 13

Wananchi mkoani Mwanza wameendelea kutembelea banda la Ofisi ya Sera, Bunge na Uratibu na kupewa elimu kuhusu masuala ya uratibu wa shughuli za Serikali ikiwemo ya menejimenti ya maafa, uwezeshaji wananchi kiuchumi katika maadhimisho ya Wiki ya Maafa ambapo Kitaifa yanafanyika Mkoani humo.

Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa Duniani inasema; “Elimu katika Kuwalinda na Kuwajengea Uwezo Vijana kwa Mustakabali Usio na Maafa”

Maadhimisho hayo yanaenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Vijana inayofanyika Viwanja vya Furahisha kuanzia Oktoba 8-13, 2024 na Kilele cha Mbio za Mwenge kitakachofanyika Uwanja wa CCM Kirumba Oktoba 1, 2024 pamoja na Kumbukumbu ya Miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itakayofanyika Kanisa Katoliki la Nyakahoja mkoani Mwanza.






Related Posts