Jukwaa la Wanawake katika Usafiri wa Anga nchini latoa elimu siku ya mtoto wa kike

Jukwaa  la Wanawake katika Usafiri wa Anga limeshiriki kusherehekea Siku ya Mtoto wa Kike Duniani kwa kutoa elimu kwa mabinti wa kike juu ya Usafiri wa Anga na fursa zilizopo katika sekta ya Usafiri wa Anga katika sherehe iliyoandaliwa na Shirika la Ndege la KLM Royal Dutch katika ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,  Terminal 3.

Akizungumza katika sherehe hizo Afisa Mtoa Taarifa za Usafiri na Usalama wa Anga Mkuu na mwanachama wa Jukwaa hilo, Annamaria Nzamba amewaeleza mabinti hao juu ya fursa nyingi zilizopo katika sekta ya Usafiri wa Anga na kuwatia moyo kuchukua masomo ya sayansi ili kuweza kuzinyakua fursa katika sekta hapo baadae na kuziba pengo la uhaba wa wataalam hasa wakike katika sekta ya Usafiri wa Anga.

Moja kati ya malengo ya jukwaa ni kuwainua mabinti wadogo walioko mashuleni kwa kuwapa elimu na kuwahamasisha kuingia katika sekta ya Anga ili kuongeza idadi ya wanawake ambayo kwa sasa ni hafifu ukilinganisha na idadi ya wanaume katika sekta.

Afisa Mtoa Taarifa za Usafiri na Usalama wa Anga Mkuu na mwanachama wa Jukwaa hilo, Annamaria Nzamba akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ikiwepo uongozaji ndege kwa baadhi ya mabinti waliofika kwa ajili ya kupata elimu kuhusu sekta ya Usafiri wa Anga ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike.

Baadhi ya mambinti wakifuatilia mada

Picha ya pamoja 

Related Posts