WAZIRI MKUU KUZINDUA WIKI YA VIJANA KITAIFA.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 11, 2024 anazindua maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa mwaka 2024 inayofanyika katika viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza.

Maadhimisho hayo ni nyenzo muhimu ya kurithisha falsafa za maendeleo za Baba wa Taifa na historia ya Taifa kwa vijana wa Tanzania.

Aidha, kupitia wiki hii Serikali na wadau wote wa maendeleo ya vijana hukumbushana wajibu wa kutambua umuhimu na mchango wa vijana katika kuleta maendeleo ya Taifa sambamba na kubaini vipaumbele vipya katika maeneo ya uwezeshaji wa vijana.

Maadhimisho hayo yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu pamoja na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar.

Kaulimbiu ya Maashimisho hayo ni “Vijana na Matumizi ya Fursa za Kidijitali kwa Maendeleo Endelevu,”.


Related Posts