MUWSA YAIMALIZA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KISHINDO,WATEJA WAAMINIFU WAJINYAKULIA ZAWADI

Na Linda Akyoo-Moshi

Ikiwa wiki ya huduma kwa Mteja inaelekea ukingongi,leo tarehe 11 Oktoba,2024 Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) imefanya ziara ya kuwatembelea wateja wake waaminifu wanaolipa Ankara zao kwa wakati na kuwapa zawadi kama motisha kwa uaminifu wao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Meneja Kitengo cha Huduma kwa Wateja Bi.Mwanandani Ally Mtonye,amesema kuwa wamehitisha wiki hii ya Huduma kwa Mteja kwa kutembelea wateja wao na kuwapa zawadi,hivyo MUWSA ina wathamini wateja wao.

Aidha Bi.Mtonye amewasisitiza wateja wa Mamlaka hiyo kulipa Ankara zao kwa wakati yaan ndani ya siku 30,na kujitahidi kuzichukulia kwa umakini ujumbe mfupi wa maandishi unaotumwa kila wakati na Mamlaka hiyo kwaajili ya kusoma mita.

Hata hivyo Bi.Mtonye amesema kuwaMUWSA imeamua kutambua na kuthamini mchango wa wateja wao katika zoezi zima la kutoa huduma bora na endelevu.

Sambamba na hilo wateja waliotembelewa na MUWSA na kupatiwa zawadi kama wateja bora,Bw.Masuwe na Bw.Chakusaga wameishukuru Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Moshi kwa kuwaamini na kuhaidi kuendelea kulipa Ankara zao kwa wakati na kutoa wito kwa wateja wote wa MUWSA kulipa ankara zao kwa wakati ili kuepusha adha ya kukatiwa maji na kukosa huduma ya maji.

Wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa wiki ya pili ya mwezi wa 10,ambayo kwa mwaka 2024 wiki hii imeangukia tarehe 07 hadi tarehe 11 Oktoba.


Related Posts