NIMESHIRIKI ZOEZI LA UANDIKISHAJI- DC MWANGA.

MKUU wa Wilaya ya Mlele Alhaj Majid Mwanga ameshiriki zoezi la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu huku akiwasisitiza wananchi kushiriki zoezi hilo.

Alhaj Majid ameshiriki zoezi hilo akiwa na viongozi wenzake ambao ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Shama Steven Peleka,Katibu wa Tawi la CCM Nelson Lunda,Mkurugenzi wa Halmashauri Sigilinda Mdemu,Katibu wa CCM Wilaya Siri Makonyola pamoja na wakaazi wenzake wa kitongoji cha Chama kijiji cha Kalovia Kata ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.

“Ninaendelea kuwasihi wananchi wa Mlele na Mpimbwe kujitokeza kujiandikisha katika siku hizo kumi zilizowekwa,”.amesema.

Related Posts