TANZANIA NA ZAMBIA WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO KURAHISISHA BIASHARA KWA WAFANYABIASHARA WADOGO

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Balozi Dkt.John Simbachawene (katikati) akisaini Maktaba wa kurahisisha mazingira ya Biashara _Simplified Trade Regime_ Hafla ya utoaji saini ilifanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Izukanji uliopo Nakonde Nchini Zambia.Kushoto mwenye Miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Mombo Mhe.Elias Mwandobe akishihudia Hafla hiyo.

…..

Tanzania na Zambia wamesaini mkataba wa makubalianno ya kurahisisha biashara (Simplify Trade Regime) kwa wafanyabiashara wadogo wanaofanya biashara ya kuingiza na kutoa biadhaa zianazozalishwa katika nchi hizo.

Makubaliano hayo yamefanyika katika Mji wa Nakonde nchini Zambia

Akizungumza kayika kikao hicho Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi John Simbachawene amesema kuwa lengo la makubaliano hayo ni kuwawezesha wafanyabiashara wadogo waweze kufanya biashara bila kufuata taratibu za wafanyabiashara wakubwa.

Katika makubaliano watatengenezewa njia yao au kuimarisha njia zao kwasababu kurahisisha wao kufanya biashara vizuri ikiwa ni pamoja na kutengeneza masoko ya pamoja ambapo wakitoka na bidhaa zao wanapita moja kwa moja bila bughuza.

“Kuwa na fomu ya forodha iliyorahisishwa rahisi simplified custom document ambapo hiyo fomu itakua sawa na Zambia kwa kuwawekea matangazo bidhaa anazotakiwa kuvusha.

“Tumekutana leo Nakonde nchi ni Zambia kwaajili ya kikao maalumu cha pande mbili kati ya Tanzania na Zambia madhumuni ya kikao ni kuweka biashara mdogo kuwasaidia waliolo kwenye mkpaka wa Tanzania na Zambia ili kuweka mazingira mazuri waeze kufanya katika mazingira mazuri

Katika mkutano huo ulioanza toka tarehe 8 mwezi huu, wataalamu waliweza kukutana kujadili na kufikia maamuzi ya pande mbili kukubaliana Kuna baadhi ya bidhaa ambazo tumezikadili nakufikia makubaliano ambozo ni 51 zitatajumuishwa katika orodha ya bidhaa ambazo zimewekwa katika utaratibu wa bidhaa ndogondogo ambazo zikishughulikiwa kwa pamoja ku wa rahisishia wafanyabiashara wadogo katika nchi zetu hizo mbili”

“Pande zote mbili ziwe na dawati malumu na kuwasaidia kuwaelimisha wafanyabiashara wadogo bidhaa, documents mbalimbali kwaajili ya kufanya biashara zao” amesema

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Methew Mkingule amesema hii ni fursa kubwa katika kipindi hiki katika mazao ya chakula na mazao mengine ya kawaida wafanya biashara wapeleke biashara Zambia kwa maslahi ya nchi yetu kwasababu ni matakwa ya nchi zetu mbili wangependa wafanyabiashara wote wanufaike wakubwa na wadogo

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Biashara na Viwanda nchini Zambia, Bi.ilian Bwalya amesema kuwa “Ni namna mojawapo yakuongeza WiGo wa wafanyabiashara kunufaika nao wanamchango mkubwa katika kuliletea Taifa mapato”

“Tulikua tumaangalia njia sahihi ya kuwafanya afanyabiashara wadogo aweze kufanya biashara kwa uhuru wakia mipakani kwa kufuata utaratibu, na kuwa na taarifa sahihi juu ya bidhaa gani zimeidhinishwa”

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Balozi Dkt.John Simbachawene (katikati) akisaini Maktaba wa kurahisisha mazingira ya Biashara _Simplified Trade Regime_ Hafla ya utoaji saini ilifanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Izukanji uliopo Nakonde Nchini Zambia.Kushoto mwenye Miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Mombo Mhe.Elias Mwandobe akishihudia Hafla hiyo.

Related Posts