HALOPESA YAADHIMISHA MIAKA NANE,YAWAFARIJI WATOTO NYUMBA YA MATUMAINI JIJINI DAR ES SALAAM

HALOPESA kupitia kampuni ya Mawasiliano HALOTEL, kuelekea siku ya maadhimisho ya Kutimiza miaka 8 katika uazishwaji wa Huduma za HaloPesa pamoja na huhitimisha kilele cha huduma kwa wateja.

HaloPesa inatambua mchango wa jamii kwa ujumla katika kufanikisha Mchango wake katika jamii.

Mnamo tarehe 11/10/2024 katika kuadhimisha siku hiyo muhimu HaloPesa imeungana kwa pamoja kutembelea Shirika la ASBAHT (Nyumba Ya Matumaini ) kilichopo Kimara Wilaya ya Temboni jijini Dar es salaam, kusherehekea kwa pamoja na Watoto wenye Vichwa vikubwa na Mgongo wazi pamoja na wazazi wa watoto hao.

Kupitia Kaulimbiu isemayo TUNAWAPENDA, TUNAWAJALI, TUNAWATHAMINI HaloPesa imeona umuhimu wa kurudisha kwa jamii katika makundi maalumu ikiwemo Watoto na katika hayo wamepeleka mahitaji maalum kama -pampas, maziwa yenye virutubisho, ungalishe utakaosaidia watoto katika lishe bora, sukari, sabuni, n.k

Lakini pia haikuishia hapo,HaloPesa walipata wasaha mzuri wa kufurahi pamoja na wazazi pamoja na watoto kupata chakula cha mchana kwa pamoja.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa HaloPesa Bw. Magesa Wandwi alisema kuwa HaloPesa inafurahi kuungana pamoja na jamii ya ASBHERT.

“Kwa hakika kwa kufika hapa tumeweza kupata elimu na uelewa kuhusu watoto hawa wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi, na tumeona jinsi wazazi watokao mikoa mbalimbali wanavyohangaika katika kituo hiki kwa ajili ya kupata matibabu kupitia hospitali ya MOI, lakini pia kuwepo hapa wanapata elimu na malezi,

Lakini pia sisi kama jamii tunahakikisha tunakua karibu na familia hizi,ikiwemo watoto hawa ambao wanaishi katika mazingira magumu ambao ni taifa la kesho.

Kwa kuona umuhimu na uhitaji wao tumeweza kuwasilisha mahitaji yao muhimu. Tunatoa wito kwa mashirika na taasisi mbalimbali ziweze kuguswa na Jamii na kufanya chochote kwaajili yao.

Aidha Mwenyekiti mtendaji Wa ASBAHT Bw Santos chuwa amesema kua anaishukuru kampuni ya huduma ya kifedha HaloPesa kupitia Kampuni ya Mawasiliano Halotel kwa ujio wake muhimu, kwani kupitia ujio wake umeweza kusaidia watoto na wazazi kupata mahitaji yao muhimu na wanaishkuru kwa upendo na kuthamini mchango wao mkubwa katika kujali watoto na familia ziishio katika mazingira haya na tumepokea mahitaji muhimu na hakika tumefurahi na kufarijika sana.

Akifuatiwa na Afisa Bidhaa na Masoko HaloPesa Bi. Aidat Lwiza alisema imekuwa ni siku nzuri na muhimu sana kwa HaloPesa. ”tumetembelea kituo hiki cha makazi ya watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi, tumepata kujifunza mambo mengi yatakayotusaidia katika maisha yetu ya kawaida,

Tumepata wasaha mzuri wa kupata chakula cha pamoja na kukabidhi mahitaji yao muhimu.

Lakini Pia tunapenda kuwaweka wazi wateja wetu na jamii kwa ujumla kua HaloPesa inathamini mchango mkubwa kwa jamii na Tunajifunza kupitia Kila tunachokiona.

Lakini pia tunatoa wito kwa jamiii kwa ujumla ikiwemo taasisi na mashirika mbalimbali kutoa mchango wao kwa jamii hasa wenye uhitaji.

kwa niaba ya HaloPesa napenda kuishukuru Shirika hili kwa mapokezi mazuri lakini pia kwa elimu waliotupatia, hakika inavutia na inahamasisha na jamii kwa ujumla kuona umuhimu katika yale yanayowaongoza.

Kwakusema hayo Sheherekea miaka 8 na HaloPesa pamoja.

HaloPesa ni maisha ishinayo!!.

Related Posts