HUDUMA YA MWENDOKASI IANZE MBAGALA’ MHE NYAMOGA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Mhe Lazaro Nyamoga imefanya ziara ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa miundombinu na uendeshaji wa mabasi yaendayo haraka

Akiongea na wananchi wa eneo la Mbagala Kijichi Mhe.Nyamoga ameitaka serikali kuhakikisha wanapeleka huduma ya mabasi katika eneo la Mbagala Kijichi ili waweze kupata huduma bora za usafiri katika eneo hilo

“Wananchi wa Mbagala wanahitaji huduma ya mabasi yaendayo kwa haraka kutokana na uwingi wa wananchi pamoja na uhitaji wa huduma hiyo, hivyo maiomba serikali iweze kutoa huduma hiyo kwa haraka” amesisitiza Kamoga

Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Zainab Katimba amesema tayari mradi umekamilika kwa asilimia 98 hivyo itaanza kutoa huduma ya usafiri katika eneo hilo

Mradi umekamilika kwa asilimia 98 hivyo tupo tayari kuanza kutoa huduma ya mabasi yaendayo kwa haraka katika eneo hili ila tunakamilisha asilimia zilizobaki” amesema Mhe.Katimba.

Related Posts